0

Watakujaje?: Moja ya kikosi cha Simba sc msimu uliopita
LIGI kuu soka Tanzania bara inaanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu kwa timu 14 kuchuana vikali kuwania taji linaloshikiliwa na mabingwa Azam fc.

Msimu ujao tutashuhudia timu tatu mpya zilizofanikiwa kupanda ligi kuu ambazo ni Ndanda fc ya Mtwara, Stand United ya Shinyanga na Polisi Morogoro.
Timu hizi zimechukua nafasi ya timu tatu zilizoporomoka daraja msimu uliopita ambazo ni Ashanti United ya Ilala, jijini Dar es salaam, Rhino Rangers ya Tabora na JKT Oljoro ya jijini Arusha.
Timu nyingine 11 zitaendelea kuwa zile zile ambazo ni Azam fc, Yanga sc, Mbeya City fc, Simba sc, Kagera Sugar, Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar, JKT Ruvu, Coastal Union, Mgambo Shooting na Tanzania Prisons.
Msimu uliopita kulikuwa na mabadiliko katika nafasi za juu. Azam walitwaa ubingwa, Yanga wakashika nafasi ya pili, Mbeya City nafasi ya tatu na Simba nafasi ya nne.
Kama unafuatilia kwa umakini ligi kuu iliyoanzishwa mwaka 1965 ikiitwa Ligi ya Taifa, baadaye Ligi Soka daraja la kwanza na hatimaye kuitwa Ligi kuu mwaka 1997 utagundua kuwa Simba na Yanga ni klabu zinazoongoza kutwaa ubingwa.
Tafsiri yake ni kwamba kocha anapoteuliwa kuiongoza Yanga au Simba, anaaminika kuipa timu ubingwa na si vinginevyo. Utawala wa Simba na Yanga umedumu kwa muda mrefu wamekuwa wakipokezana ubingwa kama vile mbio za vijiti.
Licha ya hivyo, kuna timu ambazo miaka ya nyuma ziliwahi kujitutumua na kubeba kombe, mfano Cosmopolitans FC (1967), Mseto Sports (1975), Pan African FC (1982), Tukuyu Stars (1986), Coastall Union (1988), Mtibwa Sugar (1999, 2002). Nyingine zitazitaja.

Kikosi cha Yanga sc msimu uliopita
Ubingwa wa mwisho msimu wa 2013/2014 umetua mikononi mwa timu changa ya Azam fc iliyoanza kushiriki ligi kuu msimu wa 2008/2009. Katika kipindi cha miaka sita, Azam fc wameshindana na kutwaa ubingwa. Kitu pekee kinachowasaidia wanalambalamba hao ni kuanzia pale walipoishia.
Tatizo la klabu nyingi za Tanzania hata Simba na Yanga, ni kuanza upya mara kwa mara. Ni ngumu kuona timu inaanzia pale ilipoishia. Kwa mfano timu inaweza kutwaa ubingwa msimu huu, msimu ujao ikaondoka katika ushindani wa ubingwa na kushika nafasi ya tatu au nne.
Kwa mfano 2007/2008, Yanga na Simba zilikuwa zinachuana vikali kusaka taji, lakini Azam ndio kwanza walikuwa wanacheza ligi daraja la kwanza na kupanda ligi kuu msimu huo.
2008/2009 Simba na Yanga walikuwa vidume wa kuwania taji na mwishoni wanajangwani wakatwaa kombe. 2009/2010 Simba wakiongozwa na Mzambia Patrick Phiri walitwaa ubingwa bila kufungwa mechi yoyote na wapinzani wao wakubwa walikuwa Yanga, Azam bado walikuwa wanahangaika kwa kutokea.
2010/2011 Yanga na Simba waliendelea kuchuana vikali katika mbio za ubingwa na wanajangwani kutwaa taji, lakini msimu wa 2011/2012, Simba chini ya kocha Mserbia Milovan Cirvovic walitwaa kombe tena kwa rekodi nzuri ya kuwatandika Yanga mabao 5-0.
Katika msimu huo Azam fc walishika nafasi ya pili na ndio yalikuwa mafanikio makubwa kwa klabu hiyo. Ilipata nafasi ya kucheza kombe la shirikisho barani Afrika ambapo ilifanya vizuri na kuishia raundi ya tatu baada ya kuzitoa klabu za Al Nasir Juba ya Sudan kusini, Barrack YC ya Liberia na kutolewa kwa mbinde na FAR Rabat ya Morocco.
- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=5272#sthash.LrtgeHKK.dpuf

Kikosi cha mabingwa Azam fc msimu ulioipta
Ukiangalia kwa umakini, katika msimu huu wa 2011/2012, Azam na Simba ndio walikuwa washindani wa ubingwa, Yanga walikaa pembeni kidogo.
Msimu unaofuata, 2012/2013, Azam wakaanzia walipoishia na kumaliza nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Yanga. Simba waliishia nafasi ya tatu. Kwa maana hiyo, Azam ndio waliweza kuanzia walipoishia, wakati Mnyama aliporomoka kutokana na kukosa mipango mizuri.
Katika michuano ya kombe la shirikisho, safari hiyo Azam waliteleza na kuishia raundi ya kwanza kwa kutolewa na Ferroviario ya Msumbiji.
Msimu wa 2013/2014, Azam fc wakaendeleza pale walipoishia katika michuano ya ligi kuu na wapinzani wao wakubwa wakawa Yanga na Mbeya City na hatimaye kuweka rekodi ya kutwaa kwa mara ya kwanza taji la ligi kuu.
Wapi Simba? Wao waliendelea kujikongoja na kuharibu zaidi na hatimaye kushika nafasi ya nne na mafanikio makubwa yalikuwa kubadilisha makocha tu kuanzia Milovan Cirvovic aliyewapa ubingwa 2011/2012, Patrick Liew, Abdallah Kibadeni, Zdravko Logarusic na sasa Patrick Phiri.
Kimsingi, Azam fc wamekuwa washindani wazuri kwa miaka mitatu mfululizo, wakati Simba na Yanga wanabadilishana. Kama Yanga wapo safi msimu huu, Simba wanakuwa kwenye matatizo na hivyo hivyo kwa upande wa pili.
Wagonga nyundo: Mbeya city fc walileta changamoto nzuri msimu uliopita
Ninachojaribu kueleza ni kwamba timu za Tanzania zinashindwa kuanzia pale zilipoishia katika michuano mbalimbali. Ndio maana unaweza kushangaa Mbeya City fc waliomaliza nafasi ya tatu msimu uliopita wakashuka nafasi za chini zaidi. Sio lazima iwe hivyo, wanaweza kupanda pia kutokana na maandalizi yao.
Kitu kizuri zaidi katika mpira ni kuanzia ulipoishia na unaweza kufanya hivyo kama una watu sahihi katika maeneo sahihi. Yaani una benchi nzuri la ufundi, wachezaji wazuri na utawala bora.
Uongozi katika klabu za Tanzania ni tatizo. Migogoro mingi inatokea bila sababu hasa kwa klabu za Simba na Yanga sc.
Wakati tunasubiri kuanza ligi kuu, niwakumbushe wageni Stand United, Ndanda fc na Polisi Morogoro kuwa wadau wana hamu ya kuona wanaleta ushindani wa kweli ili kuepuka ligi ya timu mbili au tatu kusaka ubingwa.
Inafahamika wazi kuwa kama timu imepanda katika misingi imara, yaani wakati inatafuta njia ya kucheza ligi kuu ilijipanga kuandaa timu badala ya kulazimisha kupanda kimagumashi, basi itaendelea kubakia ligi kuu.
 
Wakata Miwa: Kagera Sugar msimu uliopita walijitahidi kupambana, lakini walishindwa kuvuka mafanikio ya Abdallah Kibadeni
Lakini kama ujanja ujanja ulitumia, sitoi nafasi ya timu hizo kuendelea kufanya vizuri zaidi ya kurudi ligi daraja la kwanza kwa mara nyingine tena.
Mbali na hilo, nazishauri klabu kufanya maandalizi mazuri ambayo yalianza wakati wa kucheza ligi daraja la kwanza na sasa ni kuongeza nguvu ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wengine. Kama vikosi viliandaliwa vizuri kutoka ligi daraja la kwanza, kucheza ligi kuu ni kuongeza nguvu tu.
Lakini viongozi nao watambue mipaka yao. Wasipende kufanya kazi zisizowahusu. Katibu mkuu unaingiliaje mambo ya ufundi?
Na ninyi makocha bakini katika misingi ya taaluma zenu. Msikubali kuonewa na kupangiwa mambo ya ajabu nje ya kazi yenu. Huko ni kudhalilisha na kutoheshimu taaluma zenu.
Tunajua sasa hivi njaa imepungua kwa timu za ligi kuu. Kuna ‘Mihela’ kutoka kwa wadhamini Vodacom, Azam TV na baadhi ya timu zina mikataba na makampuni kama vile Binslum na TBL.
Tumieni hela hizo kiusahihi ili kuandaa timu za kushindana. Naamini mtafanya makubwa kama mipango itakuwa mizuri.

Post a Comment

AddThis

Top