0


LAKINI CHUKI YA NINI HAIKUPATA TUZO YA KTMA 2014



wazee wa ngwasuma wazee mujini wazee wa funika bovu wazee wa pamba fm academia wa pili kushoto ni VIE King Blaise na wa pili kulia ni VIE mule mule


Sio jambo la ajabu sana kuona hali hii inajitokeza eti band kubwa na inayopendwa na mashabiki wengi tanzania inakosa tuzo za KTMA.
Mmi sijui wewe pengine unajua kwanini wamekosa hata tuzo ya banad bora ya mwaka wakati band hii ina zaidi ya miaka kumi ikifanya vizuri 

Sitaki kuamini kama Fm academia hawajui kuimba wakati Jose mara aliyepata tuzo ya mwanamuziki bora wa band kafundishwa kuimba na fm academia alafu leo walimu hao ndio hawajui kuimba kiasi wakose tuzo haingii akilini

Labda ni uzalendo uliyopelekea kumpa jose mara TUZO na uzalendo wa kuwapa mashujaa musica

Kama ni uzalendo basi mbona mashujaa wanaimba muziki wenye asili ya CONGO?kwanini wasipige sindimba au ngoma za asili ya kwetu Tanzania maana tuna makabila zaidi ya 20 na yote yana asili?hapo sipati picha


Hatuongelei ushabiki ila tunatizama haki ipo wapi katika tuzo za KTMA
Sina tatizo na christian bella hapo wamefanya sawaaa kabisaaa
lakini RAPPER wake toto ze bingwa kalalamika kukosa TUZO ya rapper bora wa band hapo pia sina la kusema kwasababu kuna KITOKOLOLO

Raisi wa Fm Academia Nyoshi el Sadat na Makamu wake ambaye ni King Blaise nilipojaribu kuongea nao kuhusu jambo hili wameonyesha dharau za wazi wazi kwangu it means hawakuumia kukosa tuzo,pengine they dont know wht the meaning of TUZO au kwasabau Blog hii ipo Dodoma haipo Dar es salaam kwa hiyo wamekariri Dr es salaam ndiyo kila kitu ,,lakini cha ajabu show wanakuja kufanya dodoma na mikoa mingine kwanini wasibaki dar es salaam?,,hundred percent sijaelewa na sitaki kuelewa ila nimebaki nashangaa tu na siwezi kuacha kuandika ukweli

PENGINE dharau hizi ndio chanzo cha kukosa TUZO?mimi kama mwandishi wa habri za michezo na burudani ninahisi japo sina uhakika 

hii ni band kubwa sana TANZANI A na inakubalika sanaaaaaaa.


LIST ILIKUWA HIVI
WIMBO WA BAND
USHAMBA MZIGI -MASHUJAA
SHAMBA LA BIBI-VICTORIA SOUND
CHUKI YA NINI-FM ACADEMIA
YARABI NAFSI -MAPACHA WATATU
KIAPO-TALENT BAND







WAZEE WA PAMBA,,,vundeeeeeeeeeeeeeeeeeeee inazidi uzito tafadhali usiangusheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Post a Comment

AddThis

 
Top