0
Makamu wa raisi wa band ya fm academia Kingombe Blaise aka King blaise aka Mfalme

Mashabiki wa band ya fm academia nchini Tanzania wamesema king blaise ni kama fere gola

Kauli hiyo wametoa kwa nyakati tofauti walipoongea na mwandishi wa blog hii aliyepo jijini dar es salaam bi Flora amon 

Wamesema kwa uzoefu wao na upenzi wao katika muziki na band hasa fm academia wanaona king blaise ana uwezo mkubwa sana wa kuimba ila hana nyota kama ya fere gola

Mashabiki hao wakitolea mfano wamesema kuwa have bataringe aka Fere Golla anaimba sana lakini hakubaliki sana kama anavyokubalika fally ipupa

"fere golla anaimba sana duniani hakuna kama yeye na kwa mtu yoyote anayejua muziki hwezi kupinga hili kwasabau ndiyo ukweli,jamaa fere golla ni noma ni noma sana katika sauti na vile vile anaonekana hana maringo, huyu jamaa namfanisha na King Blaise wa fm academia yule jamaa hana maringo alafu anaimba sanaa sauti yake ni kama inatetemeka hivi alafu ni ya juu kitu ambacho wanamuziki wengi hawawezi, king blaise akitoa album yake mwenyewee nje ya band atafanya vizuri sanaa kama anavyofanya fere golla"

Hii ni kauli ya petii man wa masaki na mashabiki wengine wakimuongelea King blaise

Fere Golla ni mwanamuziki mzuri sana kutoka drc congo ambaye alishapita kwa kofi olomide akiwa muimbaji akapita kwa werason ambaye mpaka sasa anamuheshimu kama kaka yeke mzazi na hatimaye ana band yake mwenyewe 

Kwa upande wake Makamu huyo wa raisi wa fm academia king blaise alipohojiwa akasema anawaachia mashabiki kwani wao ndiyo wenye uwezo wa kujua nani anaimba nini na nani ana uwezo gani kwenye muziki yeye kazi yake ni moja tu kutoa burudani kwa mashabiki ile roho inapenda

Fm academia ni band yamiaka mingi nchini Tanaznia ikifanya muziki na kutoa burudani ya dansi

ITAZAME video ya wimbo fataki ya fm academia utunzi wake King blaise vile vile itazame video ya fere Golla hapo chini ili ujionee na kuthibitisha walichosema mashabiki hawa kutoka jijini Dar es salaam

fataki by fm academia lakini inaanza chuki ya nini alafu inafuata fataki tazama



tazam video ya Fere golla uimbaji wake na uchezaji wake



Post a Comment

AddThis

 
Top