Tim Sherwood anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha wa Crystal Palace.
Malky Mackay, ambaye aliyefanya kazi na Cardiff, jana amefanya mazungumzo kwa mara ya pili na mimiliki wa Crytal Palace, Steve Parish ili kujaza nafasi ya kocha mkuu iliyobaki wazi.
Mscotish huyo ambaye hakuwa na kazi tangu alipotimuliwa katika klabu ya Cardiff mwezi Desemba, alifanya mazungumzp zo ya awali na Parish siku ya jumapili kama alivyofanya Tim Sherwood ambaye pia anapigiwa upatu kuchukua kazi hiyo.
Parish anatazamiwa kufanya maamuzi ya mwisho juu ya kocha anayetaka arithi mikoba ya Tony Pulis ndani ya saa 48 zijazo.
Malky Mackay naye anatarajia kumrithi Tony Pulis
Post a Comment