0


Pichani:Paul Walker na ndugu yake

Waandaji wa Fast and Furious 7 wameeleza kuwa nafasi ya marehemu Paul Walker katika filamu hiyo itachukuliwa na kaka zake Celeb na Cody.

Paul Walker alikuwa akiigiza kama Brian O’Conner katika mfululizo wa Fast and Furious akiwa na timu ya mastaa wenzake kama Tyrese, Vin Diesel na Ludacris.

Katika tamko lao waliloweka kwenye ukurasa wao wa Facebook, waandaaji hao wameeleza kuwa filamu hiyo itakamilika na kutoka mwaka 2015.
Paul Walker alifariki kwa ajali ya gari November mwaka jana.

Post a Comment

AddThis

 
Top