Kocha wa mpya wa Barcelona, Luis Enrique (kushoto) ameanzisha sheria klabuni hapo.
Luis Enrique ameanzisha sheria kali kwa wachezaji wa Barcelona kuelekea msimu mpya wa La Liga.
Kocha huyo ameanika fidia watakazolipa wachezaji wake kama wataenda kinyume na taratibu zake.
Wachezaji wamepigwa marufuku kuchelewa mazoezini na kuchelewa kurudi nyumbani wakati wa usiku.
Sheria nyingi zinafanana na zile za Pep Guardiola wakati akiwa Katalunya, lakini zilikufa baada ya kutimka.
Mambo magumu: Enrique (kulia) ameanzisha sheria ili kurudia umwamba wa Barcelona na kutwaa makombe msimu ujao
SHERIA ZA ENRIQUE
Mchezaji anatakiwa kufika saa moja kabla ya mazoezi kuanza.
Wachezaji hawatakiwi kuchelewa wakati wa chakula klabuni.
Ni marufuku kunywa pombe wakati wa chakula.
Wachezaji wote wanatakiwa kuwa nyumbani kabla ya saa sita usiku siku mbili kabla ya mechi.
Wachezaji wanatakiwa kuheshimu maamuzi ya klabu.
Wachezaji wanatakiwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na Instagram
Wachezaji lazima wavae sare za klabu kwenye shughuli za klabu
Wachezaji hawaruhusiwi kujihusisha na shughuli za hatari kama michezo ya kuteleza kwenye barafu na kutumia pikipiki.
Utukutu wa kuvunja sheria unaweza kumfukuzisha mchezaji klabuni
Tata Martino alisifika kwa kuwaacha wachezaji wake huru, lakini Enrique amekuja na sheria za kuwanyoosha wanandinga wa Katalunya.
Wachezaji tayari wameanza kutekeleza sheria za kocha huyo mpya na wanaonesha juhudi katika mazoezi.
Sasa hivi wanajitahidi kumvutia kwa njia nyingine ambayo ni kukwepa kuvunja sheria zake.
Iliripotiwa na gazeti za michezo la Katalunya kuwa wachezaji watalipa fidia ya Euro 1,000 na 6,000 kama watavunja sheria za Enrique.
Fidia kubwa italipwa pale mchezaji anapovunja sheria zaidi na ataweza kaudhibiwa na uongozi wa juu wa klabu.
Na tabia sugu ya uvunjaji wa sheria inaweza kumfukuzisha mchezaji klabuni.
Haijajulikana kama kumng`ata mchezaji mwingine itaingia katika sheria ya aina hii, lakini Luis Suarez aliyesimamiswa kwa miezi minne kwa kosa kama hilo inabidi awe makini.
Michezo ya kuteleza kwenye barafu ni marufuku kwa wachezaji wa Barca
Marufuku: Enrique amewakataza wachezaji wa Barcelona kujihusisha na uendeshaji wa pikipiki.
Post a Comment