0
WAYNE Rooney ameifurahia nafasi yake chini ya kocha mpya Louis van Gaal na anaamini kuna dalili za kufanya vizuri msimu ujao zipo wazi.

Msimu uliopita, nyota huyo mwenye miaka 28 alifunga mabao 17 na kusaidia mengine 12 chini ya kocha David Moyes, lakini Man United iliishia nafasi ya 7 katika msimamo na kukosa michuano ya Ulaya.

Rooney anaamini timu yao imerudi katika makali yake chini ya Mholanzi na anasema anafurahi sana kucheza katika mfumo mpya wa 3-5-2 ambao umemfanya afunge mabao manne katika mechi tatu za maandalizi ya msimu.

“Mfumo umekuwa mzuri,” mshambuliaji huyo aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa Michigani. “Kiukweli kocha amekuja na tumekuwa tukifanya mazoezi katika mifumo tofauti, lakini ni mizuri mno, hata katika umri wangu najifunza vitu vipya na nitakuwa mzuri sana.

“Tunatakiwa kujiboresha zaidi na wiki chache zijazo, nina uhakika tutaweza. Naamini matokeo mazuri yatazidi kuja kuanzia jumamosi  (leo)”.
Manchester United itacheza na Real Madrid leo katika mechi ya michuano ya kimataifa ya kirafiki na wakishindwa watatinga fainali. Licha ya kuwa michezo ya kirafiki, Rooney anatarajia kufunga mabao na kumaliza kama vinara wa kundi lao.

“Inaweza kuwa nzuri sana kucheza na mahasimu wetu Manchester City katika mchezo wa fainali, lakini kwanza tuna mchezo na Real Madrid (leo) na ni muhimu kwetu kushinda,” Nyota huyo wa England aliongeza.


Post a Comment

AddThis

 
Top