Kwenye mahojiano hivi karibuni na kituo cha television kuhusu biashara na Branding rapper maarufu kwa kazi zake kama Black and Yellow na Work Hard Play hard ‘Wiz Khalifa’ ameongelea kufanya biashara nje ya muziki nakusema yeye huchukua pesa zake na kuwekeza mahali anapojua pana maana zaidi na kutumia vizuri nafasi anazopata kutengeneza pesa.
Kuhusu kuharibika kwa brand yake kwa sababu za kuhusishwa na makosa ya matumizi ya bangi Wiz alisema ni matatizo tu na changamoto unazokutana nazo unapokuwa kwenye biashara ya burudani duniani.
Imethibitishwa na Wiz Khalifa na kituo cha Television hicho kuwa mpaka sasa Wiz Khalifa amekamatwa mara 21 kwa makosa yanayohusishwa na Bangi. May 25 2014 alikamatwa na bangi kwenye uwanja wa ndege na hii ndio stori niliyokupa wakai huo WizKhalifaBangi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment