0
Cristiano Ronaldo, alionekana katika mazoezi huko mashiriki mwa chuo kikuu cha Michigani na anahitaji kucheza dhidi ya timu yake ya zamani ya Man United leo usiku.

CRISTIANO Ronaldo ameweka wazi kuwa ameombwa kucheza dhidi ya klabu yake ya zamani, Manchester United leo usiku katika mechi ya kirafiki nchini Marekani.
Pia nyota huyo amemuunga mkono kocha Louis van Gaal na kusema atairudisha klabu hiyo katika ushindani wa ubingwa ligi kuu soka nchini England.

Real Madrid ya Ronaldo inakabiliana na Man United kwenye uwanja wa Michigan wenye uwezo wa kuchukua watazamaji, 109,000, lakini kocha wa miamba hiyo ya Hispania, Carlo Ancelotti amesema winga huyo wa Ureno hayupo fiti kucheza.
Ronaldo amesema: ‘Tumejadiliana leo ili kunipa dakika chache za kucheza, lakini subiri tuone’.

Tayari kwa kazi: Ronaldo amesema yupo tayari kuanza kwenye mechi ya kirafiki ya kombe la kimataifa huko Michigan, ingawa kocha Carlo Ancelotti anawaza tofauti.
“Nahitaji kucheza kidogo kwasababu ni timu yangu ya zamani, kwahiyo nataka kucheza, ngoja tuone”.

Ronaldo alikuwa akihojiwa baada ya mazoezi na gwiji wa United, Paddy Crerand kwenye kituo cha TV cha klabu cha  MUTV.
Alipoulizwa kama bado anatamani kurudi Old Trafford, Ronaldo alisema: ‘Ndiyo kwa kweli, ni klabu ninayoipenda sana.
‘kila mtu anajua kwamba wakati wote ninapoizungumzia Real Madrid, lazima niizungumzie Manchester United.

“Nilipapenda pale, nilikuwa na miaka 18, nilishinda kila kitu pale, watu waliniheshimu kama Mungu mtu, kwahiyo naheshimu sana na mambo ya baadaye huwezi kujua”.
‘Ilinifanya nichanganyikiwe niliposikia bado wanaimba jina langu.

‘Nakumbuka nilipocheza dhidi ya Manchester United kwenye mechi ya ligi ya mabingwa, waliniua, moyo wangu ulijawa na furaha na ulikuwa wakati wa ajabu kwangu. Naikubali sana klabu hii, kwangu mimi ni klabu bora zaidi duniani na nina mapenzi na klabu hii”.

Hakufurahi: Ronaldo aliwaomba radhi mashabiki baada ya kuifungia Real Madrid dhidi ya klabu yake ya zamani ya Manchester United kwenye mechi ya UEFA hatua ya 16 msimu uliopita

Post a Comment

AddThis

 
Top