0
Watendaji  wa serikali za mitaa na Wakuu wa wilaya watawajibishwa kwa kushindwa kutekeleza amri ya serikali ya kuwaondoa waganga wa jadi  na mabango yanayotangaza kuwapo kwa dawa ya Ukimwi na kuchochea uhalifu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadick, aliiambia NIPASHE katika mahojiano maalumu.


Alisema kuwa Serikali imetoa muda kwa watendaji wa serikali za mitaa na wakuu wa wilaya kuondoa mabango yanayoonyesha huduma za waganga wa wajadi, ambazo zinazuia kampeni za serikali za kupambana na magonjwa kama Ukimwi kwa kuweka mabango yanayotangaza kuwapo kwa dawa za magonja hayo.


“Serikali itawachukulia hatua za kisheria watendaji wote wa serikali za mitaa maana hao ndio wanaokaa na hao waganga ikiwa ni pamoja na wakuu wa wilaya na wakuu wa vitengo vya utamaduni vilivyotoa vibali, kwa kushindwa kuwaondoa wanganga wa jadi na kuondoa mabango yao yanayochanganya wagongwa kuwa kuna dawa ya ukimwi na dengue,” alisema.


Alisema mabango ya waganga wa jadi yanachangia uhalifu kwa kuwa yanaeleza kuwa waganga hao wana dawa ya kuwapaka wahalifu ikiwa ni pamopja na kuwapa hirizi ili wasionekane na polisi wala kuchukuliwa hatua za kisheria.


Alisema kuwa zoezi la kuwachukulia hatua za kisheria zitaanza wiki ijayo kwa jiji la Dar es Salaa. Hivi karibuni Wizara ya Afya iliyapiga marufuku mabango yote ya waganga wa jadi, kwa kuwa yanapingana na kampeni za serikali za kuyanusuru maisha ya wananchi wake kwa kutoa tahadhari mbalimbali za magonjwa 

Post a Comment

AddThis

 
Top