Viongozi wa Yanga waliiongozana na timu mjini Gaborone, Botswana wamelazimika kufanya kazi ya ziada kuwakomboa uwanja wa ndege wachezaji watatu.span>
Wachezaji hao watatu
ni Amissi Tambwe raia wa Burundi ambaye alifunga mabao yote mawili
wakati Yanga ikiishinda BDF XI kwa mabao 2-0 jijini Dar. Mbuyu Twite na
Haruna Niyonzima (wote raia wa Rwanda).
Yanga imetua Gaborone kwa ajili ya kucheza mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho ikiwa ina mtaji wa bao 2-0 ilizozipata jijini Dar.span>
Wachezaji hao
walizuiwa kutokana na kuwa na uraia tofauti na Tanzania na kwa mujibu wa
sheria za Botswana walitakiwa kukatiwa visa.
Hali hiyo iliwafanya wakwame uwanjani hapo kwa takribani saa na ushee huku wengine wakilazimika kuanza msafara wa kwenda hotelini.
Baadaye suala hilo lilishughulikiwa na wachezaji hao kufanikiwa kulipiwa visa.
Post a Comment