Arsenal imelala kwa mabao 3-1 dhidi ya AS Monaco
ya Ufaransa katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kocha Arsene Wenger amekuwa akilaumiwa kwa
ubahili, akilaumiwa kwa kutumia wachezaji vijana, lakini katika mechi hiyo
alipanga mziki.
Lilikuwa ni lundo la wachezaji wazoefu ambao
walishindwa na wachezaji makinda wa Monaco.
Kikosi cha Monaco kilianza bila ya wachezaji
wake watano wa kikosi cha kwanza waliolazimika kukaa nje kwa sababu mbalimbali.
Sasa Wenger afanayeje? Sasa Wenger kweli
anapaswa kulaumiwa? Ndiyo maana alibaki kama mtu asiyejitambua wakati mechi
inaendelea na hata baada ya kwisha walipofungwa bao la tatu katika dakika za
nyongeza. Watamuua huyu mzee! hehe, Arsenal bana.
Post a Comment