Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amesema mambo
yatabadilika na kikosi chake kufanya kazi kwa uhakika lakini muda bado unahitajika.
Kopunovic amesema bado Simba ina kikosi bora
kuliko wengi wanavyofikiria.
“Kweli tumepoteza mchezo dhidi ya Stand. Hii
inatokea, kweli kutokuwa makini au kukosea ni chanzo cha kutofanya vizuri.
“Lakini kuna mambo ya kufanya, bado tunaendelea
kubadilisha. Bado tunapambana, huenda Simba wanatapwa kuwa wavumilivu.
“Sijui kabla, lakini kwa kipindi changu, mimi
naona hatujapita sehemu ndefu ambayo utasema tumeharibu sana.
“Lakini hatuwezi kuendelea au kusubiri tuharibu
tu. Tunapambana na mambo yatakwenda vizuri kikubwa waamini tunapambana na
tutaendelea kubadilisha mambo kadhaa,” alisema Kopunovic.
Post a Comment