0
Straika machachari wa Mtibwa Sugar, Mussa Hassan Mgosi, amesema hataangalia historia kuwa wameifunga mara ngapi Simba msimu huu kwa kuwa itamharibia isipokuwa atakwenda kufanya kazi siku hiyo kuhakikisha wanaifunga Simba kwa mara nyingine na kutwaa ubingwa.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Mtibwa imekutana na Simba mara tatu ambapo imefanikiwa kushinda mara mbili na kutoa sare mara moja.

Timu hizo sasa zitakutana tena kesho kwa mara ya nne ndani ya msimu mmoja kwenye fainali hiyo ya Mapinduzi inayotarajiwa kupigwa usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

 “Historia kwenye soka siku hizi si kitu cha kuzingatiwa sana, kwangu mimi nimeshafuta hiyo historia na nitaanza upya kwenye dakika 90 za kesho kwa ajili ya kuhakikisha naisaidia timu yangu ili tushinde katika hiyo fainali na tutwae ubingwa, kwa kuwa ndicho kilichotuleta huku,” alisema Mgosi.

Post a Comment

AddThis

 
Top