0
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema ana taarifa kuhusiana na viwanja vibovu.


Koponovic tokea ametua nchini hajawahi kucheza mechi katika kiwanja kibovu.

Aliiongoza Simba kutwaa kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar ambao ni safiii. Halafu akaenda kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu kwenye Dimba la Nangwanda mjini Mtwara ambalo lina moja ya viwanja vizuri vya kuchezea.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Kopunovic amesema ana taarifa ya baadhi ya viwanja kuwa hoi kwa ubovu.

"Nimeambiwa kuhusiana na hilo, hii ni Afrika nalichukulia kama changamoto.

"Usisahau nimefanya kazi Rwanda kwa miaka mitatu, kuna changamoto nyingi nimekutana nazo na huenda zikawa zinafanana na hizi zilizopo.

"Hivyo ni suala la muda tu na kujua nini cha kufanya wakati tunakabiliana nazo," alisema Mserbia huyo.

Post a Comment

AddThis

 
Top