0

Mwili wa mtu aliyeuawa na mamba katika Ziwa Baringo, Kenya mwezi December inasemekana umezikwa bila idhini ya  familia ya mtu huyo.
Inatolewa inapelekwa mahali pengine ambayo hata hatujui ni ajabu sana… Sisi tumesema tunataka mwili wa mtoto wetu, tunataka mwili wa mtoto wetu mara moja” alisema ndugu wa marehemu.
Familia hiyo iliandaa kaburi la kumzika ndugu yao lakini ikashindikana kutokana na mwili wake kukosekana katika chumba cha kuhifadhia maiti ambapo inasemekana kuwa baada ya Polisi kufika katika eneo ambalo mtu huyo aliuawa na mamba, waliwaamrisha ndugu zake wasiufuate mwili huo kwa kuwa walikuwa wakiupeleka kuufanyia upasuaji ili kuweza kubaini kifo chake, lakini baadaye ndugu walipokea taarifa ya ndugu yao kuzikwa kwenye kaburi la siri.
Mpaka sasa wazee wakasema okay chukueni miti ili ipresent huo mwili, ukiletwa  inatolewa, hatuwezi kuchimba kaburi bila mtu… hii kaburi atakula watu sasa kwetu” alisema ndugu mwingine wa marehemu.
Familia hiyo imeitaka Serikali kuingilia kati ishu hiyo na kueleza nani aliyetoa maamuzi ya kuuzika mwili wa ndugu yao.
TAZAMA Video na Audio ya taarifa hiyo kutoka katika kituo cha K24 kwa kubonyeza play.







Post a Comment

AddThis

 
Top