0
Baada ya dhiara yake Inchini GUINEA CONAKRY, ambako kadumbwiza kwenye Ukumbi wa  » ALLIANCE FRANCO CONGOLAIS « , JB MPIANA PAPA CHERI, kesha rudi JIJINI KINSHASA ambako Weekend iliyofuata  akawaburudisha Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Mpiara unaopatikana kwenye Manispaa ya  » MASINA « .

Kupitia Msemaji wake Mkuu ROGER NGANDU, JB MPIANA kasema : Stahamilini Jamani, Album yenu mnayo isubiria kwa Siku Nyingi  » BALLE DE MATCH  » Ipo njiani  kutolewa.

JB MPIANA katoa pongezi zake kwa Wasanii wenzie walio toa Albums zao mwezi uliopita, kuanzia kwa Rais WERRASON na ALBUM  » FLÈCHE INGETA « , Kijana FABREGAS na Album  » ANAPIPO « , hasa Dansi yake  » YA MADO  » inayo tikisa Kumbi nyingi Ulimwenguni, BRIGADE SARBATI  » AFFAIRE YA RANDO « , FERRE GOLA  » DÉRANGEMENT « ,

Wapo Wasanii Wengi wa CONGO ambao Albums zao zinatamba sana siku hizi, yaonyesha kwa Kiasi gani Muziki wa Congo Bado upo Juu na Watawala Ulimwengu wa Dansi. hilo ni Jambo la Maana kabisa.
Sasa Mtaona PAPA CHERI MOTO PAMBA kawaletea  » BALLE DE MATCH « , Tunawaachieni wenyewe fursa yakuona Nani Mchapa kazi na nani Bado kasinzia, Nani kaheshimu matakwa ya Mashabiki wake na nani asie yaheshimu, Mtazipata Nyimbo nyingi na nzuri, Kwenu nyie Wapenzi wa JB MPIANA Mtafurahi…

Post a Comment

AddThis

 
Top