0
Ijumaa ya Leo January 23 katika Hekaheka wamepiga story na  msanii wa Hiphop wa kikosi cha mzinga Kala Pina ambae amezungumzia mambo mbalimbali yanayomuhusu muziki, siasa na maisha yake ya mtaani.
Kwenye siasa Kala Pina  amezungumza kuwa wakati anagombea Udiwani lililopofika zoezi la  kuhesabu kura ghafla aliingiwa na kitu jichoni na kupata maumivu makali mno na kukimbilia nyumbani watu walipomuangalia hawakuona kitu na baada ya kufanya dua alipata nafuu na kurudi kituo cha kupigia kura, akakukuta mambo yameshaharibika.
Pina amesema kuwa anajitolea kuwawakilisha vijana kwa  kugombea Ubunge kupitia Jimbo la Kinondoni, lengo la kufanya hivyo ni kuweka muungano na ushirikiano kati ya vijana na wazee na kuwatetea wanyonge.
Jamaa anasema ishu ya sakata la Escrow kama angekuwa Bungeni ingebidi ngumi zitembee kama ilivyo katika Mabunge ya nchi nyingine.
Story nyingine aliyosimulia ni kisa cha kufumaniwa na wapenzi wake kilichosababisha  kutokea ugomvi  na kuamua kukimbia ili kukwepa tafrani  lakini baadae waliongea na kuyamaliza.
Akizungumzia suala la wanaume wasiopenda kuhonga wanawake wao Kala Pina amesema kuhonga ni raha kwa kuwa  kunamfanya mwanamke aepukane na vishawishi na kutulia.
Bonyeza play ili uweza kuisikiliza Hehaheka yote hapa.

Post a Comment

AddThis

 
Top