BAADA ya kudaiwa kuwa wapenzi na kisha habari hizo kufifia, hatimaye penzi la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, limeibuka upya ambapo safari hii Nay ameamua kufunguka hadharani.
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao walianzisha uhusiano wao mwishoni mwa mwaka jana na sasa mapenzi ndiyo yamekolea hadi kufikia hatua ya Nay wa Mitego kuanika hisia zake mtandaoni.
“Wamekuwa wakibanjuka kwa siri sana si unajua Nay ana mchumba wake Siwema, bado hajafanya maamuzi magumu ya kumtosa,” kilisema chanzo chetu.
Paparazi wetu alifanikiwa kunasa ujumbe wa Nay wa Mitego kwenye mtandao wa Instagram ambao ulionyesha wakiitana kwa majina ya wapendanao kuonesha dhahiri wawili hao ni wapenzi.
Mbali na kuitana huko, Nay alionesha kuwa amemmisi Wolper ambapo muda mchache baadaye naye alijibu kwa kuwa amemmisi pia kisha Nay akaifuta posti hiyo baada ya kuandamwa na maneno ya wapambe.
Mbali na kuitana huko, Nay alionesha kuwa amemmisi Wolper ambapo muda mchache baadaye naye alijibu kwa kuwa amemmisi pia kisha Nay akaifuta posti hiyo baada ya kuandamwa na maneno ya wapambe.
Kwa upande wake Nay alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Wolper na hatua ya kuunadi uhusiano wao mtandaoni huku ikifahamika kuwa ana mchumba mwingine, hakutaka kufafanua zaidi ya kujibu:
“Mimi huwa siangalii nani atasema nini wala atafikiria nini, mimi nilimmisi Wolper wangu, sikuwa na namna zaidi ya kutumia peji yangu kama nilivyofanya, tena siku hiyo alikuwa hapatikani hewani nikaamua kumtupia mtandaoni bila hofu kwani ni mtu wangu wa karibu na siogopi kitu juu yake,” alisema Nay wa Mitego.
Post a Comment