0



Katika Mahojiano yake na Mwandishi wa Habari DIEUDONNE YANGAMBA,wa Radio na TV ya Taifa ya CONGO (RTNC), KOFFI OLOMIDE, kaonekana Mwenye masikitiko kutokana na Kifo cha BABIA NDONGA CHOKORO.
MTANGAZAJI : Wote tulipigwa na Mushtuko na taarifa ya kifo cha mmoja wa Vijana wako, BABIA NDONGA CHOKORO, ambae kafariki Dunia Tarehe 08-10-2014. Kijana huyo Alie lelewa na kukuzwa kimuziki na Wewe. Ulipokeaje Habari hiyo ya Masikitiko!!!
KOFFI OLOMIDE : Kabla yayote, nawatolea Salamu zangu kwawale wote wanao tufwata kwa Wakati huu popote pale mlipo. iwe Ulaya, Africa, na kwengineko.
Ninayo Majonzi na Uchungu Mkubwa kutokana na Kifo cha  » BABIA NDONGA CHOKORO « , Mimi mwenyewe nilikua napenda kumuita  » PETIT SARKOZY « . Leo hii kafariki Dunia, na bila shaka hiyo ndo njia yetu sote. Apumzike kwa Amani. Taarifa ya kifo chake nimeipata kutoka ANGOLA, ambako ndiko alikochagua nakuweka Maskani yake.
Kifo chake kimetokea wakati Dada yake KISINDJORA akiwa jela, Ila yote ni kazi yake MUNGU, Tulimpenda sana yeye kampenda zaidi. Salamu zangu za Rambi rambi ziwaendee Wapenzi wote wa Group QUARTIER LATIN, kadhalika Kwa Familia ya Marehemu, Wanae (PRINCE), na Mkewe.
Kama sijakosea, Mazishi yake yaandaliwa Jumamosi ijayo, Tarehe 25-10-2014, Hatuna Mda Mrefu kwa Mimi kuongelea Mema yote ambayo kayatenda BABIA NDONGA wakati bado akiwa nasi kwenye GROUP QUARTIER LATIN. Alikua mmoja kati ya Vijana waliokua na Sauti nzuri ya Uimbaji kwenye Group letu.
MTANGAZAJI : MEJA GENERALI CELESTIN KANYAMA, ambae ndie Mkuu wa Jeshi la Polisi JIJINI KINSHASA, katoa Onyo kali dhidi ya nyinyi wanamuziki,hasa kutokana na Tabia yenu ya Malumbano, Kakemea vikali baadhi ya vitendo vya WASEMAJI wa WANAMUZIKI, visivyo endana na Maadili ya Umma !!! Kasema Sheria itafwata mkondo wake, bila kujali Umri wala Hadhi ya Mtu atakae kwenda kinyume.
KOFFI OLOMIDE : Kwanza Shukrani zangu za dhati zimwendee GENERALI KANYAMA kutokana na kauli yake isio na Utata dhidi yetu sisi Wanamuziki. Ujinga umekua mwingi sana hadi Tunaonekana Watu wasio faa. Chuki imesha jipandikiza kwenye Nyoyo ya Wengi kati yetu. Itakua vizuri pale tuu Onyo hilo la GENERALI litakapo fwatiwa na Vitendo !!!
Ntaendelea kumshukuru GENERALI KANYAMA kwa kitendo cha kukemea wale WASEMAJI wasiokua na Maadili yeyote yanayo endana na kazi hiyo, Watu hao huongea vitu vingine vilivyo tofauti kabisa na maelekezo ya ma BOSS wao. Tunaweza tukachukua Mfano wa MSEMAJI MKUU WA SEREKALI Mheshimiwa LAMBERT MENDE, anapo ongea na Waandishi wa Habari, hua hakosi Karatasi, huku akiongea Maneno kwa Mpangilio, Anaongea kwa umakini nakuonekana Mtu mwenye Maana. Sasa kwa hawa WASEMAJI wetu, wameshaigeuza kazi hiyo kama Dili,Wanatafuta kwanza manufaa yao binafsi.
Kwani nikila Siku, kila Wiki ambayo hua tunatoa Album ? Nawala sio kila Siku ambayo hua tunafanya SHOO. Sasa nashangaa kila Siku Tunawaona Mkiwaalika kwenye Vipindi vyenu,na hakuna Jipya wanalo liongelea, bali Hadithi ni ileile ambayo tuliyo kwisha izoea ( ALBUM ITATOLEWA HIVI KARIBUNI, ALBUM IPO NJIANI NAKADHALIKA ).
Jamani, hata Msemaji wa Rais OBAMA, anapo hojiana na Waandishi wa Habari, Utamuona akiwa na Karatasi, anaongea kwa ufasaha na yaliyo yamuhimu. Sio Hawa MASEMAJI WETU namambo yao ya kurupuka ,kuongea yale yasiyo na maana.!!!
MTANGAZAJI : Naona wamtaja RAIS OBAMA, wacha basi tugusie kidogo Habari za Kimataifa, hasa zile zinazo husiana na Ugonjwa wa EBOLA. RAIS OBAMA kamteuwa Wakili RON KLAIN kama   » MR EBOLA  » ambae kampa Majukumu ya kupambana na Virusi vya EBOLA, Wengi husema RAIS OBAMA kafwatilia nyayo zako, kwakua Wewe ndie Mtu wa kwanza aliekubali kuitwa Jina hilo la  » MZEE EBOLA «
KOFFI OLOMIDE : Kweli kabisa, na katika harakati zangu za kuwaunga mkono Waathirika wa Ugonjwa huo, Naandaa SHOO kabambe Tarehe 02-11-2014 Kwenye Ukumbi wa ROMEO GOLF. SHOO yenyewe naipa jina la  » MZEE EBOLA « .
Kama ilivyo kawaida yangu, Ninapo ongea kitu, hua najitaidi kujua Undani wa mada niiongeleayo. Sijui Wale walio nipachika Jina hilo la  » MZEE EBOLA  » walikua na dhamira Nzuri au mbaya dhidi yangu, ila Jina hilo Mimi nalikubali. Ni Mtu gani huyo alie na haki yakumcheka mwenzie kwa kosa lakukutwa na Virusi vya EBOLA ? Kila mmoja wetu anaweza akajikuta kwa njia moja au nyingine kesha ambukizwa na Virusi vya EBOLA.
Waweza ukawa Mtu na afya yako nzuri, na mapesa zako, Nguo zako hunyooshwa vizuri, Saa na Pete nzuri Mkononi,nakadhalika,Swali Je Ikiwa Mtu alie kupigia nguo zako Pasi anavyo Virusi vya EBOLA, huoni kama uwezekano ni mdogo sana kwawewe kusalimika ?.
Unaweza ukawa na Girlfriend wako, huko aliko kwa bahati mbaya kakutana na Mtu alie na EBOLA, Endapo akija kwako Mkajikuta mkiwa pamoja, basi jua uwezekano ni mkubwa sana kwako wewe kuambukizwa. Yamaanisha hakuna atakae Salimika kutokana na Nguvu ya Virusi vya EBOLA.
Hakuna anae ruhusiwa kumcheka Mgonjwa, awe yule kaumwa EBOLA, UKIMWI, au maradhi mengine, na kwanini kumcheka ? ni Magonjwa kama mengine.
Wale ambao leo hii wanaathirika na magonjwa hayo wanahitaji msaada wetu.
Nimepata Fursa yakuongea na Waziri wa Afya, kujua ni mbinu gani itumiwe ili kupambana vilivyo na Magonjwa hayo, na jinsi gani yakuwasaidia wale walioathirika.
Mimi nimekubali kuwa MASCOT wa Wagonjwa wa EBOLA, na naitikia pia kuitwa  » MZEE EBOLA « . Nilipatwa na Furaha paletuu nilipo sikia kwamba RAIS OBAMA kamteua Mtu na kampa jina la  » MR EBOLA « , yamaanisha tunaendana sambamba.
Ninao mpango wakukutana hivi karibuni na Mabalozi wa Inchi za SIERRA LEONE, LIBERIA, GUINEA, kujadiliana nao, nakuwaonyesha Mshikamano wangu kwao, wajue ya kwamba tupo pamoja.
SHOO yangu ya Tarehe 02-11-2014, Kipato cha pesa kitakacho tokana na SHOO hiyo, ntakigawa mara mbili, pande moja ntatoa kama mchango kwa Waathirika wa Ugonjwa wa EBOLA.
Nifanyavyo hivyo, sio katika Harakati ya kibiashara hapana, naonyesha moyo mwema wakutaka kusaidia.

Post a Comment

AddThis

 
Top