0
Habari zilizo tufikia punde, za ashiria kwamba Hali ya afya ya Mzee LUTUMBA SIMARO MASIYA yaendelea kua mbaya,
Kutokana na Vyanzo vyetu vilivyo kwenye Wizara ya Mambo ya Inje ,Hatua za Haraka zilichukuliwa ili Msanii huyo Mkongwe apelekwe Ulaya kwa uchunguzi zaidi wa Afya yake.
Wahudumu wa Wizara ya Mambo ya Inje, waliitwa kwa haraka sana Juzi Alhamisi Tarehe 23-10-2014  kwenye maeneo ya saa Saba Mchana ilikulishughulikia Swala la MZEE LUTUMBA. Boss wa Orchestra  » BANA OK « .
Baada ya Kikao cha dharura Wizarani hapo, Maofisa walitumwa kwa haraka kwenda kumchukua MZEE LUTUMBA nyumbani kwake JIJINI KINSHASA, kwenye Barabara ya ISANGI Manispaa ya LINGWALA.
Yaani ni swala la MaSaa kadhaa zilizo saliha, Ili MTUNZI MKUU huyo wa Nyimbo awekwe kwenye Ndege akielekea Barani Ulaya kwa Matibabu na Huduma sahihi na ya uhakika.
Kutokana na Sababu za kiafya, MZEE LUTUMBA kaomba radhi kwakutokuonekana kwake Sherehe ya Kumbukumbu ya kuadhimisha Miaka 25 tokea afariki  » LE GRAND MAITRE LUAMBO MAKIADI « .
Siku chache baadae, MZEE LUTUMBA alitembelewa Nyumbani kwake na MAWAZIRI WAWILI waliokuja kumjulia hali. Mheshimiwa NAIBU WAZIRI MKUU na WAZIRI WA BAJETI  » DANIEL MUKOKO SAMBA « , akiongozana na WAZIRI WA AFYA Mheshimiwa FELIX KABANGE NUMBI « .
Wakati akiwapokea Ma Waziri hao, MZEE LUTUMBA SIMARO MASIYA kasema, kafarijika zaidi na kuwepo kwao hapo,  » Ninavyo waona ni dawa tosha kwangu, najisikia Nafuu.
Ma WAZIRI hao, wamesema ya kwamba hawaelewi kabisa msimamo wa Serekali, kwanini hua inatumia Pesa nyingi wakati wa Msiba wa WANAMUZIKI, pahali pakuwasaidia wakati bado wapo Hai.
MZEE LUTUMBA yuko kwenye Matayarisho ya Album yake  »  ENCORE ET TOUJOURS « , itakayo tolewa hivi karibuni. Mwezi waNane katupia kwenye Soko la Muziki Single  » MA PRIÈRE «
Tunaendelea kuzifwatilia habari kwa ajili yenu.

Post a Comment

AddThis

 
Top