MFAHAMU REDDY AMISI MWIMBAJI NA MTUNZI WA NYIMBO ZILIZO PENDWA
Kwajina halisi Anaitwa NYAMWISI NGOY, Maarufu kwa Jina REDDY AMISI Aka BAILO CANTO.
Kazaliwa JIJINI KINSHASA Tarehe 05-05-1960. Katokea kwenye Familia ya Watoto 8.
REDDY AMISI Anae Mke na Watoto 6.
Kaikumbatia Fani ya Muziki tokea Mwaka 1975 pale alipojiunga na Group la Kwaya la Kanisa Katoliki » CHEM CHEM YETU » akiwa kama Muimbaji. Mwaka Mmoja Baadae kaja kujiunga na Group » SAMBOLE » iliokua ikiongozwa na MAITRE NGOMBE.
Katika Harakati zake za kujiendeleza kimuziki, REDDY AMISI kahamia kwenye Group Mbalimbali ya Vijana JIJINI KINSHASA, Zikiwemo : Group » JUVÉNILE » Mwaka 1977, Group » LIKAMWISI » Mwaka 1978, Group » TOUCHE PAS DE LINGWALA » Mwaka 1980.
Nikwenye Group hili la Mwisho, Ndipo REDDY AMISI kakutana na KOFFI OLOMIDE, ambae kajakutokea kuwa Mdhamini wake. Ndie kampeleka hadi kwa PAPA WEMBA, na Baadae kakubaliwa kujiunga na Orchestra VIVA LA MUSICA Tarehe 04-10-1982. Akiwa kama Mwimbaji na Mtunzi wa Nyimbo.
Mara tuu baada yakukubaliwa na kuorodheshwa kama Mwimbaji kwenye Group VIVA LA MUSICA ya Mkongwe PAPA WEMBA, REDDY AMISI kaonyesha Umahiri wake wa Uimbaji, Jambo lililo pelekea akubalike Zaidi na mashabiki kadhalika na Wapenzi wa Muziki kwa Jumla.
REDDY AMISI kafaanikiwa kutoa Wimbo wake wa kwanza » KOTIDA » Wimbo ambao ukapelekea apendwe kwakiasi kikubwa na Umma, Ndipo zikaja kufwatia Albums zilizo na Ubora wa kipekee :
1. ZAKINA ( 1988 )
2. QUEEN LINA ( 1990 )
3. INJUSTICE ( 1992 )
4. PRUDENCE ( 1994 )
5. ZIG ( 1997 )
6. ÉTOILE ( 1999 )
7. FIN D’EXIL ( 2001 )
8. COMPTEUR à ZÉRO ( 2003 )
9. LIGNE DROITE ( 2006 )
10. LIKELEMBA ( 2010 ) .
REDDY AMISI katokea kuwa Kijana wakaribu, Mwaminifu pia mwenye Kupendwa sana na PAPA WEMBA, wakati Mzee huyo alipochukua uamuzi wa kuhamia JIJINI PARIS ( FRANCE ) Mwaka 1987 wala hajamuacha REDDY AMISI, kamshawishi waongozane wote kwa pamoja.
Wakiwa tayari JIJINI PARIS, REDDY AMISI kawa mmoja wa Watu walio changia kwakiasi kikubwa kuundwa kwa Orchestra » VIVA LA MUSICA INTERNATIONAL » , » VIVA LA MUSICA COUR DES GRANDS » , » MOLOKAÏ STARS « .
Ndie pia aliekua chanzo cha kuundwa Orchestra » NOUVELLE ÉCRITURE « , Group Alilonalo PAPA WEMBA hadi leo
Ingawa bado wanao uhusiano mzuri katiyao, REDDY AMISI kaonyesha dalili za kujitegemea, baada ya Miaka 20 akiwa kwenye Group VIVA LA MUSICA, kasema kesha komaa kimuziki, na kampa taarifa hizo PAPA WEMBA ambae kwa upande wake hajaweka pingamizi lolote.
Leo hii REDDY AMISI ni Mmiliki na Kiongozi wa Group lake mwenyewe » CASA DO CANTO » .
Post a Comment