0
ASERNE Wenger anaamini Alexis Sanchez aliathirika kama anavyoathirika Neymar wakati akiwa Barcelona kutokana na uwepo wa Lionel Messi.

Asernal ilitumia Euro milioni 40 kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile majira haya ya kiangazi na leo hii anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya.
Licha ya kucheza kama winga akiwa Barca, Alexis atachezeshwa kama mshambuliaji Emirates na Wenger anaamini atang`ara zaidi katika nafasi hiyo kutokana na kutokuwepo kwa ‘mchawi’ wake Messi.
“Kwa mara ya kwanza alitinga katika rada zangu alipokuwa Udinese na baadaye Barcelona”. Alisema Mfaransa huyo alipozungumza na The Dail Mirror.

“Ni mshambuliaji. Ni mmaliziaji mzuri ambaye alikuwa na kiwango kizuri Italia. Nilimuona pale na alikuwa amesimama vizuri. Lakini mambo yalikuwa magumu alipoenda Barcelona kama ilivyo kwa Neymar sahizi”.
“Unapomuona Neymar wa Brazil na Neymar wa Barcelona sio mtu mmoja. Naamini kuwa Alexis anaweza kucheza kushoto, kulia na mbele na ndio maana nilimfuata”.


Post a Comment

AddThis

 
Top