0
Wiki chache zilizopita mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo alitangaza ujio wa mavazi yake mapya kupitia label yenye ufupisho wa jina lake ‘CR7 lakini biashara yake hiyo inaweza kupata tatizo nchini Marekani.

Kuna uwezekano mkubwa Ronaldo akashindwa kuuza mavazi yake yenye lebo ya ‘CR7′ Marekani baada ya mtu mmoja nchini humo kufungua kesi dhidi ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid kutokana na matumizi ya nembo ya “CR7″.

Christopher Renzi ambaye alilisajili jina la “CR7″ kibiashara (akiunganisha herufi za kwanza za majina yake na tarehe yake ya kuzaliwa: 7th October) nchini Marekani 2009 kwa matumizi ya website yake pamoja na label yake ndogo ya mavazi, aliandikiwa barua mara kadhaa na kampuni ya JBS Textile Group inayotengeneza bidhaa za ‘CR7′ za Cristiano Ronaldo, wakimwambia aache kutumia nembo hiyo.


JBS pia wameiandikia barua ofisi ya usajili wa nembo za kibiashara ya Marekani ili waweze kuwapatia haki ya kutumia jina nembo hiyo nchini humo lakini pamoja na hilo, 

Renzi nae amefungua kesi dhidi ya JBS na Ronaldo  ili aweze kutajwa kisheria kabisa kuwa mmiliki halali wa leseni ya nembo ya ‘CR7kwenye mipaka ya Marekani.
Kwenye maongezi na shirika la habari la Marekani Reuters, mwanasheria wa Renzi alisema “Tunachohitaji na wao kutuacha huru bila usumbufu

Post a Comment

AddThis

 
Top