0


Upinzani wa jadi ni kitu cha kawaida sana kwenye mchezo wa soka duniani kote, Tanzania kuna Simba vs Yanga, Uingereza kuna Manchester United vs Liverpool, Misri kuna Al Ahly vs Zamalek, nchini Hispania kuna kubwa kuliko ambayo inaingiza mpaka mambo ya kisiasa FC Barcelona vs watoto wa mfalme Real Madrid.

Uhasama wa Real vs Barca ni mkubwa sana kiasi cha hivi juzi nchini Marekani wakati wa mechi ya maandalizi ya msimu mpya kati ya AS Roma dhidi ya Real Madrid, mizimu ya El Clasico iliingilia mchezo huo wakati mchezaji wa zamani wa FC Barcelona Seydou Keita alipokataa kushikana mikono na mchezaji wa Madrid – Pepe na kisha akamrushia chupa ya maji kichwani kabla ya mechi.

Tukio hili lilipelekea wachezaji wengine wa timu hizi mbili kuwatenganisha wachezaji hao, Xabi Alonso akimtuliza mzuka Keita ambae alimtuhumu Pepe kwa kumuita nyani kwenye mchezo wa kwanza wa Spanish Supercopa mwaka 2011.
Kwa mujibu wa Fox broadcast, kamisaa wa mchezo alikaririwa akisema kwamba Pepe alimpiga kibao Keita kwenye ugomvi huo.
Unaweza kuangalia video ya ugomvi wa Pepe vs Keita hapa chini…


Post a Comment

AddThis

 
Top