0

Ingawa kashindwa kutamka kwa uwazi kana kwamba Kajiondoa kwenye Group ” JET SET ” ya FERRE GOLA, Dalili zaonyesha uwezokano mkubwa kwa CHIKITO kutaka kujitegemea mwenyewe.

Kutokana na Mahojiano kati yake na Mtangazaji AICHA OKOKO, CHIKITO kasema kwa wakati huu,yeye hutizama kwanza Maisha yake ya hapo Baadae. Kwa mtazamo wake,hajaona mafaanikio kamili kwa kipindi cha miaka 9 aliokaa akiwa na FERRE GOLA.

Kutokana na sababu hiyo, CHIKITO kachukua Uamuzi wakuingia Studio akiwa kwenye matayarisho ya Album ” BOMBE HIROSHIMA “itakayo tolewa mwishoni mwa mwaka huu.

Alipo ulizwa na Mtangazaji AICHA OKOKO swali lakutaka kujua kana kwamba Kajiondoa rasmi kwenye Group ” JET SET LES GAULOIS ”  inayo ongozwa na FERRE GOLA, CHIKITO kashindwa kujibu kiufasaha, katoa majibu ambayo hayaendani kabisa na Swali kwakusema ” WANACHO KISUBIRIA WATU KWA SASA NI ALBUM BOMBE ATOMIQUE “. Album ambayo kutokana na maelezo yake itakua bora zaidi na itapokelewa vizuri na Mashabiki wake.
KAULIZWA NDIZI ANAJIBU ANAJIBU MANANASI YAANI SWALI NA JIBU HAVIENDANI 

CHIKITO, katoa Mfano wa Kijana ambae bado yuko Nyumbani kwao akiishi na Mama yake Mzazi,Pindi anapo gundua Mambo hayaendi vizuri kwa Hapo Nyumbani,ni wajibu wake kutaka kujitegemea hadi kufikia kuchukua Uamuzi wakuondoka Nyumbani kwao na kuhamia sehemu nyingine.


CHIKITO kaendelea kusema kua,Mtoto Mmoja anaweza kuondoka Nyumbani na kuyaanza maisha yake ya Pekee,hilo linaeleweka, Sasa endapo Watoto watatu huchukua Uamuzi kama huo tena kwa wakati mmoja, sasa hapo ninani atakae laumiwa? Mzazi au Watoto.

Mtangazaji AICHA OKOKO wala hajamuachia CHIKITO kaendelea kumbana na maswali, Kamrudisha kwanza kwenye Historia yake mwenyewe kwa kusema : ( CHIKITO, WEWE NI MTU ULIE LELEWA NA FERRE GOLA,KAKULETA KWENYE GROUP LAKE UKIWA BADO MDOGO, WOTE TUMESHUHUDIA HILO,LEO HII KWELI WAWEZA KUMSALITI FERRE GOLA ?).

CHIKITO kamjibu kwakusema : Kadri Umri unavyo zidi kusonga mbele, Ndipo pia Mabadiliko makubwa hujitokeza maishani mwa Mwanaadamu. Ndio, Nakubali kweli Nimeanza Muziki nikiwa Mdogo, Ila kwa wakati huu Mimi sasa ni Mtu Mzima, na siko radhi tena kudangwanywa tena kwa kupewa PIPI.

Kwa sasa Mimi CHIKITO nimesha elewa Mambo ya ulimwengu huu jinsi yalivyo, Wakati sasa wawadia kwa mimi kuonyesha Kipaji changu na Uwezo nilionao, Kwangu mimi Muziki upo kwenye Damu.

AICHA OKOKO kaendelea kumshushia CHIKITO, kamwambia Aibu ilioje kwako wewe kujiondoa kwa FERRE GOLA, bila hata kumtaarifu, ukachukua uamuzi wa kusafiri kutoka JIJINI KINSHASA na kwenda INCHINI ANGOLA kimya kimya,wala hujachukua fursa ya kuomba hata Hati yako ya kusafiria.

CHIKITO kamjibu kwa kusema : ” MWANA MAYELE AYEBAKA KO PRÉPARER LOBI NAYE / MTOTO MJANJA NA MWENYE AKILI NI YULE AMBAE ANAJUA KUJIAANDAA KWA AJILI YA MAISHA YAKE YA YA BAADAE.

Sina lolote la Ubaya nitakalo liongelea lihusianalo na huko niliko tokea. Majibu kutokana na maswali yote mliyonayo, na ambayo yana husiana na Mimi, Mtayapata kwenye Album ” BOMBE HIROSHIMA “.

Swali la Udadisi la Mtangazaji AICHA OKOKO kutaka kujua kama CHIKITO yuko na mpango wa kujiunga na WENGE MUSICA MAISON MÈRE, CHIKITO KAKATAA KABISA KWA KUSEMA WALA HANA MPANGO HUO. 

Kaendelea kusema, Kipaji alicho nacho ndicho chawafanya watu kujitokeza na kutaka kumsaidia na kumsapoti, kati yao akiwemo Mdhamini Mkubwa wa GROUP WENGE MUSICA MAISON MERE anae julikana kwa Jina la GERVAIS NFUTILA LIYEBO.

AICHA OKOKO kamwambia kwa mara nyingite CHIKITO kuwa YEYE NI MTU ASIEKUA NA SHUKRAN,BAADA YA MIAKA 9 KWENYE GROUP LILILO KULEA NA KUKUJALI HADI UKAPELEKWA ULAYA,UKAPEWA FURSA YA KUIMBA JIJINI PARIS KWENYE UKUMBI WA ZENITH.

Jibu la CHIKITO ni kwamba, NI SAHIHI KABISA, NIMEKAA HUKO KWA KIPINDI CHA MIAKA TISA, KWANI NYINYI MLIKUA MKIPENDELEA NIKAE HADI MIAKA 30? WAKATI MIMI NIKIWA SINA KITU ? IKITOKEA LEO HII MUNGU AEPUSHIE MBALI KIFO KINANIKUTA, NANI YULE ATAKAE WAJALI WANANGU?

NAOMBA NIPENI NAFASI PIA NA WAKATI ,NDIPO MTAKAPO GUNDUA KIPAJI CHANGU!!! MNIELEWE KAMA MULIVYO WAELEWA WENGI KABLA YANGU. 

WAKATI NDO HUU WAWADIA KWA CHIKITO KUDHIHIRISHA KIPAJI CHAKE.
KAMALIZIA KWA KUSEMA YEYE HAYUPO FB,WALE AMBAO WANATUMIA JINA LAKE FB NI MATAPELI.

MTU AKITAKA KUWASILIANA NAE BASI AMTAFUTE KWENYE NAMBA HIZI 00243997838041 / 00243822954474.

*** KAMA WIKI MMOJA ILIOPITA, MSEMAJI MKUU WA WERRASON, SANKARA DE KUNTA akiwa kwenye Ndege JIJINI PARIS, KATIKA MAHOJIANO YAKE NA MTANGAZAJI PAPY GENE, KASEMA UHAKIKA ALIONAO NI KWAMBA, PINDI CHIKITO ATAKAPO MALIZA SHUGHULI ZAKE HUKO ALIKO INCHINI ANGOLA, ATAKUJA MOJA KWA MOJA KUJIUNGA NA GROUP WENGE MUSICA MAISON MERE .

Post a Comment

AddThis

 
Top