0
Jerry Tegete, Geilson Santos, na Andrey Coutinho ni wazi wataingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha Maximo katika michuano ya Kagame Cup, ambayo itaanza kutimua vumbi lake wikendi hii nchini, Rwanda.

Watakaporudi Saimon Msuva na Mrisho Ngassa kutoka katika majukumu ya timu ya Taifa itawabidi wapambane ili kurudisha nafasi zao katika kikosi cha kwanza. SAfu ya nyuma inapangika lakini katika idara ya kiungo  bado kuna wasiwasi wa ni mfumo gani ambao utaifanya timu kucheza katika usawa na kutoa matokeo.

 Si kila mchezaji anayeachwa au kutemwa katika klabu za Simba SC na Yanga SC si mzuri. Wapo wachezaji ambao huachwa japokuwa kiufundi ni wachezaji bora, ila wapo pia ambao wanaachwa kwa sababu za nje ya uwanja, inaweza kuwa sababu za kinidhamu au mahusiano mabaya na baadhi ya viongozi. Mathalani kulikuwa na sababu yoyote ya msingi kwa Yanga kumuacha, Athumani Iddi ‘ Chuji’ ?.
 Ndiyo inawezekana zikawepo sababu nyingi tu za kumuondoa Chuji nje ya kikosi cha Yanga baada ya kuichezea klabu hiyo kwa kipindi cha miaka saba. 
Chuji ameondoka Yanga kwa sababu ya historia ya nyuma, ila mchezaji huyo alikuwa mkimya na kufanya kazi yake ipasavyo ndani ya uwanja.

 Tangu alipoachwa ghafla na Yanga katikati ya mwaka 2011, kiungo huyo wa kati alionekana kutuliza akili yake na kucheza mpira kitu ambacho kilimfanya kupandisha upya kiwango chake na kupelekea kuwemo katika timu ya Taifa kwa miaka miwili mfululizo.

 Hadi anaondoka Yanga katikati ya mwaka huu kiungo huyo alikuwa sehemu ya wachezaji wa Taifa Stars. Yanga imeachana na Chuji huku mchezaji huyo akiwa amekomaa kiakili na kupevuka kiuchezaji. Chuji ameachwa Yanga kimakosa ndiyo maana kocha wa sasa, Marcio Maximo ameanza ‘ kum-set’ mlinzi Mbuyu Twite kucheza kama kiungo wa ulinzi. 

Hiyo ni dalili kuwa hakuna kiungo sahihi wa nafasi hiyo miongoni mwa viungo waliopo. Salum Telela anaweza kucheza kwa ufasaha nafasi ya kiungo wa ulinzi. Uwezo wake katika kushambulia ni wa kiwango cha juu ambacho unaweza kumlinganisha na Chuji.

 Telela ni mzuiaji mzuri wa nafasi na mkabaji asiyechoka lakini ni mchezaji ‘ mwenye bahati mbaya’. Hajawahi kutulia ndani ya Yanga kutokana na kuandamwa na majeraha yasiyokwisha. 
Kiwango cha juu alichokionyesha katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Agosti, 2013 dhidi ya Azam FC ikiwemo kufunga bao la umbali ambalo liliwapa taji hilo Yanga kilibeba matumaini makubwa kuwa mchezaji huyo aliyekuwa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja angeimarisha safu ya kiungo na kufanya Mwalimu kuwa na machaguo ya kutosha.
 
Jerryson Tegete (kulia)  na Marcio Maximo ni marafiki wa siku nyingi
Lakini siku chache baadae akaumia kwa mara nyingine. Maumivu ya Telela ni kama yale ya kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Arsenal, Abou Diaby. 

Telela ni mchezaji mzuri ila si wa kumtegemea moja kwa moja kwa moja kutokana na majeraha yake yasiyokwisha. Kama atakuwa safi Yanga hawataliona pengo la Chuji, ila ikiwa tofauti timu hiyo itapata wakati mgumu.

 Usajili wa Yanga ni mzuri kwa kuwa, Mwalimu amekuja na wachezaji anaowafahamu. Andrey Coutinho na Jaja ni wachezaji wa nafasi za mbele, huku Omega akirudi ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Frank Domayo.

Nani ni kiungo sahihi-namba sita katika timu ya Yanga?. Mbuyu anaweza jukumu hilo lakini, je, ataweza kutimiza majukumu yote muhimu, hilo si jambo la kutegemea moja kwa moja kutoka kwake. Anaweza kucheza vizuri na kutimiza majukumu yote ya ukabaji na kuziba njia za hatari za timu pinzani, ila anaweza kusumbuliwa katika upigaji wa pasi za kuanzisha mashambulizi kwa viungo wachezesha timu. 

Kupokea pasi kutoka kwa walinzi na kuipitisha katika njia sahihi ni moja kati ya sifa muhimu za kiungo wa ulinzi, Chuji na Domayo waliweza kutimiza majukumu hayo japo si kwa asilimia zote. Kitendo cha kuwapoteza kwa wakati mmoja wachezaji hao ni tatizo japokuwa Maximo anaweza kuja na mfumo mpya. 4-3-3 unaweza kuwapa tabu. 

Kwanini nasema hivyo, Mbuyu si mzuri katika kusogoea mbele na mpira jambo ambalo litawalazimu viungo wengine wawili kushuka chini zaidi hali ambayo itawafanya wachezaji wa safu ya mbele kushuka hivyo kuharibu mfumo. Ili usawa uwepo katika upangaji wa timu, Maximo atahitaji kuwajaza mastaa wake uwanjani na mfumo pekee unaoweza kuwafanya kutulia uwanjani ni 4-3-3.


Mshambuliaji wa Yanga, Mbrazil,  Gleison Santos Santana ‘Jaja’. Picha na Global Publisher
 Maximo amekuwa akisisitiza upigaji wa krosi, majukumu ambayo hutakiwa kufanywa na walinzi wa pembeni. Dan Alves ameweza kuendana na mfumo huo katika klabu ya Barcena na kufanya majukumu yote ya upigaji wa krosi. 

Lakini anakuwa na uhuru wa kufanya hivyo kwa sababu kiungo wa ulinzi ni mtu anayeweza kulinda nafasi zote za nyuma upande ambao mpira huwepo. Ndivyp anavyocheza Sergio Busquets. 

Si tu ni kungo mwenye majukumu ya kuunganisha timu kutoka safu ya nyuma na ile ya kati, bali pia ni mlinzi mzuri. Yanga wanaweza kuishi bila Chuji lakini wanaweza kujifunza kutoka kwa kocha wao msaidizi, Salvatory Edward ambaye tangu kuondoka kwake katika timu hiyo hakujatokea kiungo aliyekamilika ndani ya dimba la kati kama yeye.

James Chilapondwa, raia huyio wa Malawi alisajiliwa na kocha Jacky Chamangwana katikati ya miaka ya 2000, alionekana kama mzuri zaidi namba nane kuwahi kuichezea Yanga lakini majeraha yakazima matarajio yote ya mashabiki wa klabu hiyo. James alikuwa akipiga pasi za mbali, pasi safi za mwisho na kufunga mabao ya mbali.

Mtindo wa uchezaji wa Yanga umebadilika katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Tangu kuwasili kwa Haruna Niyonzima, Yanga imekuwa ikicheza pasi nyingi za kutandaza uwanja huku wakisonga ,mbele. 

Hawategemei sana mabao ya mbali kwa kuwa wana uwezo wa kucheza hadi ya maeneo ya hatari ya timu pinzani, ila wanapobanwa mbinu mbadala hutumika na kurudi katika mchezo wa kuwanya pasi ndefu. Ikiwemo kupiga krosi nyingi.

 


Post a Comment

AddThis

 
Top