0
Mdhamini wa mashindano ya Hepautwa cup 2014, Nuru Hepautwa akikagua timu ya kata ya Gangilonga katika uzinduzi wa  mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Samora

Mdhamini wa mashindano ya Hepautwa cup 2014,Nuru Hepautwa akikagua timu ya kata ya Makorongoni katika uzinduzi wa  mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Samora

Sehemu ya heka heka zilizofungasha virago vya Gangilonga  kama inavyoonekana pichani

 KINYANG’ANYIRO cha kugombea kombe la Hepautwa  limezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki kwa mpambano kati ya  kata ya Gangilonga na Makorongoni kwa kushuhudiwa Gangilonga  kushushiwa kipigo cha aibu kwa kufungwa magoli 6 -0 katika  mtanange ulioshuhudiwa na mamia ya mashabiki wa soka mkoani  hapa na kufanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa.  
 Mechi hiyo ya upande mmoja mchezaji Michael Gabriel kuwa  nyota wa mchezo baada ya kufunga magoli manne pekee yake na magoli mengine yakifungwa na Leonard Geka na David Mhanga  katika mchezo ambao ulichezeshwa vema na refarii Bakari  Makupa  Mvua ya magoli kwa kata ya Gangilonga ilianza mnamo dk.11  kwa mchezaji David Mhanga kufunga goli kwa mkwaju mkali  baada ya kuelewana vema na Michael Gabriel aliyeisumbua  ngome ya kata ya Gangilonga walionyesha mapema kuzidiwa  katika mchezo huo.

Nyota wa mchezo huo Michael Gabriel alianza kuishushia mvua ya magoli Gangilonga katika dk ya 28 kwa kufunga goli la  pili na katika dk 38 alifunga goli la tatu na kuwapa matumaini kata ya Makorongoni kujihakikishia nafasi ya kuingia katika makundi ya nane bora.

 Mnamo dk. 42 Michael Gabriel kwa kutumia juhudi binafsi  alimzidi kete beki wa Gangilonga Abdalah Adebayo kwa kumpiga chenga ya maudhi na kuipatia kata ya Makorongoni goli la nne na kuwakatisha tamaa ya kata ya Gangilonga ‘watoto wa geti  kali’ na kufanya hadi kwenda mapumziko wakiongoza kwa magoli 4 kwa sifuri.  

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa kata ya Gangilonga kutaka kurudisha lakini bahati haikuwa yao na mnamo dk 47 ya  kipindi cha pili mchezaji Leonard Geka aliipatia kata ya  Makorongoni goli la tano na dk ya 79 Michael Gabriel  alifunga goli la sita na kuwahakikishi timu ya Makorongoni  nafasi ya kuingia katika hatua ya makundi.  Awali wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mgeni rasmi Nuru  Hepautwa ambaye ndiye mdhamini wa mashindano hayo alisema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuibua vipaji vipya  katika kata 16 zinazounda halmshauri ya manispaa ya Iringa  na kupiga vita janga jipya la maambukizi mapya ya virus vya  ukimwi.  
Alisema alisema mashindano hayo yatasaidia kukua kwa soka  ndani ya mkoa wa Iringa na  kukuza viwango vya vijana kuwezesha ajira na pia kuepukana na ugonjwa wa Ukimwi na  kuwaweka katika afya njema vijana ambao kwa sasa wamekuwa  wakikiuka maadili kwa wengi wao kujiingiza katika makundi  hatarishi yakiwemo ya watumiaji wa madawa ya kulevya.  

 Katika mechi nyingine za mtoano zilizoendelea juzi na jana  kata ya Mlandege iliumana vikali na kata ya Ilala na mlandege kufanikiwa kuwaondoa Ilala kwa bao 1 – 0  Mchezo mwingine ulikuwa kati ya kata ya Isikalilo dhidi ya  kata ya Ruaha ambapo Ruaha imeaga mashindano baada ya  kufungwa magoli 5 – 4 hivyo Isakalilo imesonga mbele na  kusubiri kuingia katika makundi ya timu nne nne.  
Katika mashindano ya Hepautwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kombe na sh.1,000,000  na sh.600,000 kwa  mshindi wa pili na sh 300,000 kwa mshindi wa tatu na  mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kila mwaka mkoani  hapa.


 

Post a Comment

AddThis

 
Top