INAWEZEKANA lisiwe jibu sahihi lakini kwa kiasi fulani linatoa picha juu ya kinachoendelea kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, kila kona gumzo ni juu ya nani mkali kimuziki kati ya Diamond Platnumz dhidi ya Ali Kiba.Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiye staa kwa sasa na amedumu kileleni kwa miaka kadhaa, hilo halina ubishi, lakini Ali Kiba amerejea kwa kutoa nyimbo mbili za Kimasomaso na Mwana baada ya ukimya wa miaka kadhaa, ukijumlisha vijembe ambavyo wanapigana wawili hao kwenye vyombo vya habari, gumzo limekuwa kubwa juu ya nani ni mkali kati yao kimuziki.
Ali Kiba ambaye anatarajiwa kufanya shoo yake ya kwanza kubwa tangu aliporejea, katika Tamasha la Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Agosti 8, 2014, ameonekana kuongoza kwenye kura za maoni juu ya nani mkali kati yake na Diamond kupitia kuraza za mitandao ya kijamii zikiwemo Twitter na Facebook.
Diamond Platnumz
Alipoanza kusika wengi waliamini angepotea kama ilivyotokea kwa wengi, lakini amedumu na kuwa msanii mkubwa, kazi zake na wasanii wa nje zimemuongezea thamani na ameonekana kuwa mwenye thamani kubwa zaidi kuliko wengine katika Bongo Fleva. Anastahili pongezi kwa kuendelea kubaki kileleni kwa miaka zaidi ya mitatu.
Ali Kiba
Sauti yake ndiyo silaha kubwa, alikuwa msanii mkubwa kiasi cha kuimba wimbo mmoja na R. Kelly ambaye naye alikiri kushangazwa na uzuri wa sauti ya kipekee ya Kiba. Hakutoa wimbo kwa miaka mitatu lakini bado hakujishusha thamani kila alipotakiwa kwenye shoo, amerejea, anadai kiti chake hakikuwa na mtu, ila kilikuwa na vumbi, sasa anakipangusa na kukaa mwenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment