0


CHRISTIAN MBEMBA MAARUFU KWA JINA LA SAVANET DEPITCHO, KAZALIWA  TAREHE 12-10-1970 JIJINI KINSHASA


YEYE NI KIJANA AMBAE MALENGO YAKE YALIKUA HAYAENDANI KABISA NA MASWALA YA MUZIKI, KWAKUA KAWA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU JIJINI PARIS, AMBAKO KASOMEA MASWALA YA POLYTECHNIC.

KAJIUNGA RASMI NA MUZIKI KWENYE MIAKA YA 1991 AKIWA NA GROUP  ”  WENGE  EL  PARIS  ” KWA WAKATI ULE IKIONGOZWA NA  ROI PELE MARIE PAUL
MWAKA 1997 KAJIONDOA KWENYE GROUP  WENGE  EL  PARIS, NA KASUBIRIA  MWAKA 1998,NDIPO KACHUKUA UAMUZI WA KUJIUNGA NA GROUP ” QUARTIER LATIN ” YA KOFFI  OLOMIDE AMBAKO KAKAA HADI MWAKA 2000.

MWISHONI MWA MWAKA 2000, KAPATWA NA WAZO LA KUTAKA KUJITEGEMEA MWENYEWE, SAVANET DE PITCHO ” RONALDO ” ,KAJIONDOA KWENYE GROUP QUARTIER LATIN, NA KUUNDA GROUP LAKE ” BARAKA CONFORT,HOLLYWOOD ” .

KWA SASA YUKO KWENYE MATAYARISHO YA ALBUM ” ISRAEL  NYOSO PETE ” ITAKAYO TOLEWA MWEZI UJAO.

KWENYE ALBUM HIYO,KAPATA USHIRIKIANO WA KOFFI OLOMIDE, BENICO POPOLIPO,LAOLYTE LASSA,OLIVIER TSHIMANGA, NA WENGINEO …

MBALI NA MASWALA YA MUZIKI ,SAVANET DE PITCHO MASKANI YAKE NI JIJINI ZURICH  NCHINI SWITZERLAND AMBAKO ANAISHI NA MKEWE BRIGITTE,WAKIWA NA WATOTO WAO SABA!!!.

Post a Comment

AddThis

 
Top