0

SERGE MOVILI MAZANI MAARUFU KWA JINA LA CELEO SCRAM, NI MWANAMUZIKI REPA KUTOKA NCHI YA CONGO DRC.

KAZALIWA JIJINI KINSHASA TAREHE 03-04-1978. KAMA BAADHI YA WENGI WA VIJANA KATIKA JIJI HILO, CELEO SCRAM,KAANZA MUZIKI KATIKA VIKUNDI VYA MTAANI,KABLA YA KUJIUNGA KWA MDA MFUPI NA PAPA WEMBA.

JINA LA CELEO SCRAM,LAANZA KUFAHAMIKA ZAIDI WAKATI KAJIUNGA NA GROUP WENGE MUSICA MAISON MÈRE YA WERRASON NGIAMA MAKANDA MWAKA 1997, BAADA TUU YA KUSAMBARATIKA KWA GROUP WENGE MUSICA ASILIA!!!.

MWANZONI,ILIMJIA VIGUMU KABISA ILI KIPAJI CHAKE KIPATE  KUDHIHIRIKA, NI BAADA YA KUJIONDOA KWA REPA MASHUHURI BILL CLINTON KALONDJI MWAKA 2004, NA NDIPO KACHUKUA USUKAMI WA KIKOSI CHA MAREPA, AKISAIDIWA NA REPA ” ROI DAVID “.

USHIRIKIANO WA MAREPA HAO, HASA KWENYE GENEREC YA ALBUM ” ALERTE GÉNÉRALE ” ILIFANYA WAFAANIKIWE KUPEWA TUZO KWENYE KORA AWARDS YA MWAKA 2005 INCHINI AFRICA YA KUSINI .

KUTOKANA NA MAWASILIANO MABAYA YALIYO JITOKEZA KATI YAKE NA BOSI WAKE WERRASON, CELEO SCRAM KAJIONDOA RASMI KWENYE GROUP WENGE MUSICA MAISON MÈRE MWAKA 2007, NA KUUNDA GROUP LAKE BINAFSI NA KALIPA JINA LA  ” PLUS 10 ” .

BADO TUKIWA TUNASUBIRIA ALBUM YAKE YA TATU ” ICI C’EST PARIS ” ITAKAYO TOLEWA HIVI KARIBUNI “, CELEO SCRAM KESHATOA ALBUM MBILI ZILIZO POKELEWA VIZURI SOKONI :

1.NZOTO NA NZOTO MWAKA 2008
2.YES WE CAN  MWAKA 2012

Post a Comment

AddThis

 
Top