NAHODHA wa timu ya Taifa ya Ghana, ‘Black Stars’, Asamoah Gyan ameongeza mkataba na klabu yake ya Al Ain mpaka mwaka 2018, klabu imetangaza kwenye tovuti yake rasmi.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Sunderland alibakisha miaka miwili katika mkataba wake wa miaka minne, lakini nyota huyo mwenye miaka 28 ameongeza mkataba jana alhamisi.
Gyan kwasasa amefikisha magoli sita katika kombe la dunia baada ya kufunga nchini Brazil na kuwa mchezaji wa Afrika aliyefunga magoli mengi zaidi ukanda huu .
Kitendo cha kuongeza mkataba na klabu hiyo ya Garden City, Gyan amejisikia furaha na kuelekeza nguvu zote huko.
“Nimefurahi sana kuongeza mkataba wangu mpaka 2018 , naishukuru bodi ya klabu, uongozi na mashabiki wote kwa kuniunga mkono,” Gyan aliiambia Tovuti ya klabu.
“Nimekuwa na furaha tangu nilipowasili 2011, nina matumaini ya kuisaidia klabu kushinda makombe”.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana, ambaye awali alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo mwaka 2011, amefunga magoli 82 katika mechi 66 za ligi alizocheza.
Post a Comment