0


Hawatoki:  Juventus ipo makini kuwabakisha wachezaji wake muhimu ikiwa ni pamoja na kiungo wake, Arturo Vidal (kushoto).
NYOTA wa Juventus na Chile,  Arturo Vidal amekanusha taarifa za yeye kujiunga na Manchester United, kwa mujibu wa ripoit nchini Italia.

Vidal amekuwa akihusishwa kuondoka Turini majira haya ya kiangazi, ambapo klabu za Man United na Real Madrid zikitajwa kuiwania saini yake.
Lakini alipoulizwa kuhusu hatima yake, Vidal alisema: “Siendi Manchester”.

Vidal aliwasili Italia baada ya likizo na alipoulizwa na waandishi wa habari kama atabaki Juventus alisema: “Siendi Manchester. Naweza kusema nitabakia Juve? Sijui.
“Nitazungumza na Allegri jumatatu na tutaona. Sijazungumza na Allegri au mchezaji mwenzangu yeyote yule, lakini siendi Manchester.
Gazeti la Italia la Gazzetta Dello Sport pia liliripoti kuwa Juventus hawataki kumuuza kiungo huyo aliyebakisha miaka mitatu katika mkataba wake-lakini wanaweza kushawishika na dau la Euro milioni 45 (Paundi milioni 36). 
Kwenye rada: Nyota wa kimataifa wa Chile, Vidal kwa muda mrefu anawindwa na  Louis van Gaal   
Maisha mapya: Manchester United wana matumaini ya kujijenga upya chini ya Louis van Gaal.
Gazeti hilo pia liliripoti kuwa Liverpool na Asernal zinaitaka saini ya Vidal.
Taarifa za Vidal kukataa kujiunga na Man United zitamkata maini bosi wa timu hiyo ambaye kwa muda mredu anamhitaji ili kuimarisha safu ya kiungo, licha ya kumsajili Ander Herrera kutokea Atletico Madrid.
Vidal alijiunga na Juve mwaka 20011 akitokea Bayer Leverkusen na amefunga mabao 11 katika mechi 32 alizocheza na kuisaidia miamba hiyo ya Turini kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo msimu uliopita.

 

Post a Comment

AddThis

 
Top