Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Francis Alhamisi ya July 24 2014 nchini Italia amekutana na Meriam mwanamke wa Sudan ambae alihukumiwa kunyongwa nchini Sudan kwa kosa la kuolewa na mume Mkristo mwaka 2011.
Meriam na watoto wake wawili akiwemo huyu wa mwisho aliezaliwa gerezani pamoja na mume wake ambae ni raia wa Marekani mwenye asili ya Sudan, waliwasili Italy wakiwa wameongozana na Afisa wa Italia ambae alisaidia kwenye mazungumzo na serikali ya Sudan ambayo iliwashikilia Meriam na mumewe kwa wiki kadhaa baada ya kuwakamata Airport wakiondoka nchini humo.
Video iliyotolewa na Vatican imemuonyesha Pope akimpa Meriam medali pamoja na rozari ambapo baada ya kukutana na Pope, wawili hawa wakiwa na watoto wao watambatana kuelekea nchini Marekani ambako ndiko makazi yao yalipo New Hampshire alikowahi kuishi mume wa Meriam.
Afisa wa Italia aliehusika kuongea na serikali ya Sudan ili familia hii iachiwe, amesema ilibidi wawe wapole kwenye maongezi na ndicho kilichosaidia mwishoni wakaachiwa huru baada ya kushikiliwa pamoja na kwamba Mahakama kuu ya Sudan ilimuachia huru Meriam.Meriam mwenye umri wa miaka 27 alihukumiwa kifo baada ya kukataa amri ya kurudi kwenye dini ya baba yake ambae ni Muislamu ambapo alifungwa gerezani na kujifungulia mtoto wake wa pili hukohuko akiwa amefungwa minyororo mpaka miguuni wakati wa kujifungua.
Waziri wa mambo ya nje wa Italia Federica Mogherini akiwa na mtoto wa Meriam wakati wakiwasili nchini Italy July 24 2014 baada ya kuachiwa huru Sudan.
Post a Comment