0

Mwisho wa maisha Chelsea: Frank Lampard anajiunga na  New York City FC.
Frank Lampard anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mchezaji mpya wa  New York City FC leo majira ya saa 9.30 alasiri.

Mkutano na waandishi wa habari umetangazwa mjini New York kwa ajili ya kutambulisha mchezaji mpya na anatarajiwa kuwa nyota wa zamani wa Chelsea.
Tukio hilo litafanyika Brooklyn Bridge Park, ambalo pia litamhusisha Lampard kufundisha vijana 40 wa kliniki ya  watoto ya Marekani.
Lampard alishinda makombe matatu ya ligi kuu, makombe manne ya FA na makombe mawili ya ligi na moja la UEFA (pichani juu).

Lampard alimaliza mkataba wake na Chelsea mapema majira haya ya kiangazi na hajaongezewa kandarasi nyingine.
 


Post a Comment

AddThis

 
Top