0
Neyma Kwenye Cover La Jarida La Time
1] Kabla ya Barcelona, Neymar ameichezea klabu moja tu ambayo ni Santos. Hii ilikuwa baada tu ya kutoka kwenye shule ya soka ya Santos aliyojiunga nayo mwaka 2003 akiwa na miaka 11.

2] Alifunga goli lake la 100 kwenye maisha yake ya soka tarehe 5 February 2012, ilikuwa siku yake ya kuzaliwa na alikuwa anafikisha miaka 20.

3] Real Madrid walitaka kumsajili toka akiwa na miaka 14,walifatilia maisha yake ya soka mpaka kumpa dili,Neymar alipitia mambo yote mpaka vipimo vya afya ila mwaka 2011 ilishindikana kwenda Real pale Santos walipotoa pesa nyingi zaidi kumbakiza Brazil.

4] West Ham ndio klabu kubwa ya kwanza kutaka kumsajili Neymar baada ya kuona kipaji chake, Ilikuwa tayari kutoa paundi milioni 12, ndio chanzo cha Neymar kutambulika kama mchezaji wa kimataifa zaidid,ikafwatiwa na Chelsea.

5] Neymar alikosa namba kwenye kikosi cha timu ya taifa ya brazil ya kombe la dunia la mwaka 2010 kilichopangwa na Dunga, hakuwepo hata kwenye wachezaji wa dharura ingawa Pele na Romario walipendekeza awepo.

6] Neymar amekuwa baba akiwa na miaka 19,mtoto wake wa kwanza wa kiume anaitwa David Lucca na mpaka sasa Neymar hajaijulisha dunia mama wa mtoto ni nani.

7] Neymar ni mchezaji wa tisa kwenye orodha wa wachezaji wa Barcelona walionunuliwa kwa ada kubwa zaidi. Ada yake ya uhamisho ni €57 million.

8] Ukizingatia wachezaji wakali wanaotoka Brazil, Neymar ndio mchezaji wa kwanza wa Brazil kukava jarida la Time, Na Wabrazil wengi waliokava jarida hili ni wanasiasa.

9] Neymar alivyojiunga na Barcelona alipewa dili linalomlipa dola milioni 74 ndani ya mwaka mmoja, mwaka 2012 alitajwa kuwa mchezaji wa saba tajiri zaidi duniani huku jarida la Forbes likimtaja kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani mwenye miaka chini ya 25. Kwa sasa ni wa sita kwenye wanasoka na wanamichezo matajiri zaidi duniani.

10] Mwaka 2012  na 2013 Neymar ametajwa kuwa mchezaji anayeuza zaidi akiwekwa kwenye matangazo na Jarida la SportsPro na kuwafunika wachezaji kama Ronaldo, Messi,Rory McLlroy na Usain Bolt.


Post a Comment

AddThis

 
Top