0

Arsene Wenger akipozi katika picha na nyota wa  New York Red Bulls, Thierry Henry (wa pili kushoto).

KOCHA wa Asernal, Mfaransa,  Arsene Wenger ameweka wazi kuwa wachezaji wake watatu walioshinda kombe la dunia wana uwezekano mkubwa wa kukosa mechi ya ufunguzi ya ligi kuu soka nchini England dhidi ya Crystal Palace.
Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski wapo likizo mpaka Agosti 11 mwaka huu baada ya kuisaidia Ujerumani kutwaa kombe la dunia nchini Brazil.
Nyota hao watarudi London zikisalia siku tano tu kabla ya kuanza ligi dhidi ya kikosi cha Tony Pulis. 
Wachezaji wa Asernal wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa  New York Red Bulls kuelekea mechi ya kirafiki kesho jumamosi.  
  Wenger wachezaji wake watatu washindi wa kombe la dunia wanaelekea kukosa mechi ya kwanza ya msimu.
Mfaransa huyo alisema: “Nimewapa likizo nzuri kwasababu nina uzoefu na wachezaji waliokuwa katika fainali ya kombe la dunia. Unahitaji kupumzika”.
“Watakuwa tayari?  Mertesacker anajiandaa vizuri – lakini kwa mchezo wa kwanza Agosti 16 sidhani kama watakuwa tayari”.
Wenger aliyekataa kuthibitisha kama amemuadhibu Jack Wilshere baada ya kupigwa picha akivuta sigara, pia aliwaibukia FIFA na kuwaambia wanatakiwa kufirikia upya ratiba yao kwasababu imempa ugumu katika kikosi chake.

Abou Diaby akijiweka fiti kwenye mazoezi mjini New York
 

Post a Comment

AddThis

 
Top