0
Kwenye ishu ya mahusiano msanii wa Hiphop Future ana sifa ya kuwa na watoto wanne hivi sasa na wote wana mama tofauti. Kabla na uhusiano na Ciara alikuwa tayari na watoto watatu lakini wote aliwaacha na hivi sasa inasemekana imefika zamu ya Ciara.

Tetesi zinasema kwamba Future alikuwa ameachana na Ciara hata kabla ya kujifungua mtoto na hivi sasa anaonekana kuwa karibu sana kimapenzi na mbunifu wake wa mavazi anaitwa Tyrina Lee.

Future ameonekana akiwa na mwanamke huyo kila sehemu akiwa kwenye tour, sehemu za mapumziko hadi maisha ya huyo mwanamke yamebadilika akifanya shopping za gharama na vyanzo vinasema ni pesa za Future.

Tangu Ciara ajifungue mtoto, Future anatumia muda mdogo sana kwenda kumuangalia mwanae lakini muda mwingi wanatumia kuwa na Tyrina Lee. Ukitembelea ukurasa wa mwanamke huyo kwenye instagram kuna picha nyingi akiwa na Future ndani ya hotel au kwenye ndege ya tour.


Post a Comment

AddThis

 
Top