0


Watu 17 wamekufa na wengine 56 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya moro best kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la pandambili wilaya ya kongwa mkoani Dodoma

Ajali hiyo mbaya kabisa imetokea leo majira ya saa mbili asubuhi ambapo basi hilo la kampuni ya Moro Best lenye namba za usajili T258 AHV lilikuwa likitokea mpwapwa kuelekea Dar es salaam likagongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T820 CKU na tela lake namba T390 CKT likitokea Dar es salaam kuelekea Dodoma

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma kamishna mwandamizi David Misime amesema kati ya waliokufa wanaume ni 12 na wanawake ni 5

Miongoni mwa waliokufa ni dereva wa basi hilo Saidi Lusogo na kondakta wake,pamoja na dereva wa lori Golbert Nemanywa
Wengine waliofariki kwenye ajali hiyo ni Merina Mericeli mkazi wa Mpwapwa,Chritina mkazi wa Mpwapwa,Nasib Mkazi wa Machenje KOngwa pamoja na Wilson Suda mkazi wa mpwapwa



Wengine waliyopoteza maisha ni Mark Masawe mkazi wa Mpwapwa,Gabriel Majachiwipe, na JuSTINE Maksi mkazi wa Mpwapwa

Kamanda Misime amefafanua kuwa,majeruhi wamelazwa katika hospitali za Wilaya ya Kongwa na hospitali ya rifaa ya Dodoma

Kamnda Misime amesema kuwa chanzo ch ajli hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita gar linguine na kwenda kuligonga basi hilo 



Post a Comment

AddThis

 
Top