0


Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadick, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Farough Baghozah na Wajumbe, Evarist Hagila na Saad Kawemba

MAANDALIZI ya ziara ya magwiji wa Real Madrid ‘Real Madrid Legends’ yamezidi kushika kasi ambapo leo kamati ya maandalizi imemtembelea mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidy Mecky Sadick, ofsini kwake, Ilala Jijini Dar kwa lengo la kumueleza rasmi tukio hilo la kihistoria litakalofanyika mwezi ujao.
Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake, Farough Baghozah ilikutana na mkuu huyo wa mkoa ambaye alifurahiswa na jambo hilo litaloweza kufungua fursa mbalimbali ikiwemo kuutangaza utalii wa Tanzania anga za kimatifa.
Menenja wa ziara hiyo, Dennis Ssebo amesema kwamba walikaribishwa kwa heshima na mkuu wa mkoa na kuahidi kuwapa ushirikiano mkubwa, huku akiwa mwenyeji wa magwiji hao wanaokuja kwa mara ya kwanza barani Afrika.
“Tumepokelewa vizuri na mkuu wa mkoa. Umetukaribisha kwa heshima zote na ameahidi kutupa ushirikiano mkubwa,” Alisema Ssebo.
Magwiji hao watatua nchini Agosti 22 mwaka huu na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi maalum cha nyota wa Tanzania Agosti 23 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ssebo alisema mechi hiyo itatazamwa kwa kiingilio cha chini kabisa cha shilingi elfu tano na wanaamini watanzania wengi wataweza kumudu kwasababu wamepewa taarifa mwezi mmoja kabla.
Miongoni mwa wachezaji hao waliopata kutamba katika michuano ya La Liga, UEFA na kombe la dunia ambao watatua nchini ni pamoja na Luis Madeila Figo, Zidedine Zidane, Fabio Cannavaro, Roberto Carlos , Ronaldo de Lima, Michael Owen na wengineo.
Baada ya mechi ya kirafiki, magwiji hao watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini na kupanda Mlima Kilimanjaro, jambo ambalo litaonwa na watu wengi zaidi duniani kwasababu hata Real Madrid TV itakuwepo kurekodi tukio zima.
Ujio wa magwiji hao ni mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake, Farough Baghozah.

Post a Comment

AddThis

 
Top