0
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzaania bara, Azam fc wamegonga mwamba kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu unaotarajia kuanza kushika kasi Saptemba 20 mwaka huu.

Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga alisema wamewasiliana na kocha mkuu wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi kuomba kucheza mechi ya kirafi mkoani Mbeya au Chamazi, lakini imeshindikana kwasababu wao wameamua kupumzika.
“Tumewasiliana na Mwalimu Mwambusi kuomba kucheza nao mechi ya kirafiki, lakini imeshindikana kwasababu ametueleza kuwa baada ya ligi kusogezwa mbele wameamua kupumzika. Kwahiyo hawaendelei na mazoezi”. Alisema Jafar.
“Tunacheza mechi za kirafiki kwa lengo la kocha mkuu Joseph Marius Omog kutazama kama wachezaji wake wanaelewa mafundisho yake”.
Azam ambao leo hii asubuhi walishinda bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Chamazi wamedhamiria kuomba mechi ya kirafiki na wekundu wa Msimbazi Simba.
Jafar alisema tayari wameshaongea na makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange` Kaburu` na amewaambia atatoa jibu siku  chache zijazo.
“Kama kuna uwezekano tunataka kucheza na Simba, Tumeshaongea na Kaburu na kutueleza kuwa atatujibu. Kama watakuwa tayari, sisi tuko tayari muda wowote kucheza nao”. Alisema Jafar.

- See more at: http://shaffihdauda.com/?p=4084#sthash.3AMzXk3L.dpuf

Post a Comment

AddThis

Top