0
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta (aliye na mpira) akifanya vitu vyake dhidi ya Msumbiji mwishoni mwa wiki iliyopita.

Na Shaffih Dauda, Dar es salaam
KATIKA maisha ya kawaida tu, kila mtu anapenda kuheshimika na kuthaminiwa na mtu mwingine. Hakuna anayependa kudharauliwa kwa namna yoyote ile. Heshima ndio kila kitu.
Mtu anapopewa thamani yake ni jambo jema na la kufurahisha. Hata katika masuala ya kazi, bosi anapoonesha kujali, kuheshimu na kuthamini kazi ya mfanyakazi, basi huongeza ufanisi wa kazi na kuwapa motisha zaidi waajiriwa.
Kwa kuwathamini wafanyakazi wako, ni namna nzuri ya kujipatia mafanikio kwa kampuni au taasisi yoyote ile. Watu watakuwa na morali ya kufanya kazi na kujitolea ili kukulipa fadhila.
Wachezaji wa soka ni miongoni mwa watu wanaoheshimika zaidi duniani. Leo hii nani asiyemthamini Cristiano Ronaldo nchini kwao Ureno au Lionel Messi  nchini Argentina, Neymar kwa Wabrazil? Hawa ni watu wanaothaminiwa sana kwa kazi yao ya kucheza kabumbu.
Thomas Ulimwengu (kulia) aliwachachafya mabeki wa Msumbiji
Messi anaposafiri kwa ndege kwenda kwao Argentina kwa ajili ya kuitumikia timu ya taifa, shirikisho la nchi hiyo linamkatia tiketi ya daraja la juu kama sehemu ya kuthamini ujio na kazi yake.
Unajua kwenye ndege kuna madaraja ya tiketi. Utapata ‘Economy Class’ na ‘Business Class’. Kwa waliobahatika kupanda ndege wanafahamu madaraja haya vizuri.
‘Economy Class’ ni kwa watu wa kawaida tu, lakini ‘Business Class’ ni kwa watu fulani wa heshima, hata bei ya tiketi yake imechangamka kidogo.
Juzi juzi, wachezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu, wanaokipiga  klabu ya TP Mazembe nchini DR Congo pamoja na Mwinyi Kazimoto Mwitula anayecheza klabu ya Al Markhiya ya Qatar walikuja nchini kuitumikia Taifa Stars.
Stars ilikuwa inakabiliwa na mchezo muhimu wa kuwania kufuzu hatua  ya makundi kusaka tiketi ya kushiriki fainali za mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morrocco ambapo mechi ya kwanza ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2 ndani ya uwanja wa Taifa,  julai 20 mwaka huu.
  

Kiungo wa Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto (katikati)
Katika mechi hiyo, Samatta, Mwinyi na Ulimwengu walianzishwa na kocha Mart Nooij. Sasa wanajiandaa kwa mechi ya marudiano itayopigwa uwanja wa Taifa wa Zimpeto mjini Maputo kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu.
Sasa stori iliyopo kwasasa ni kwamba wakati wanandinga hao wa kimataifa wanasafiri kuja Tanzania, shirikisho la soka Tanzania, TFF chini ya Rais Jamal Emil Malinzi liliwafanyia kitu cha thamani kubwa ndani ya ndege a.k.a  Pipa.
Samata, Ulimwengu na Mwinyi  walikatiwa tiketi za `Businness Class` kama ambavyo wachezaji wote wa ukweli duniani wanasafiri ndani ya ‘Business’. Yaani walisafiri kama vile Messi, Ronaldo, Neymar, na wachezaji wengine wakubwa.
Hali hii imewafurahisa sana akina Mbwana na kuwapa motisha kubwa ya kuitumikia Taifa Stars.
Wamejisikia kuthaminiwa sana, kiasi kwamba wamepata morali ya kufanya kazi nzuri. Hawajawahi kupandishwa ‘Business Class’ na inavyosemekana ndio utakuwa utaratibu ili wasichoke.
Unajua kwenye business Class unaweza kulala kwa raha ili kupunguza uchovu wa safari.
Hapa TFF mmefanya jambo zuri la kuwathamini wanandinga wa kimataifa.
Kila la kheri Taifa Stars kuelekea kwenye mechi ya marudiano mjini Maputo nchini Msumbuji.

Post a Comment

AddThis

 
Top