BEKI mkongwe wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini Louis van Gaal ni mtu sahihi kukabidhiwa majukumu ya ukocha mkuu klabuni hapo.
Kutangazwa kwa Mholanzi huyo kama mirthi wa David Moyes kulistishwa jana alhamisi ili kumuacha huru wakati huu akiiandaa timu ya taifa ya Uholanzi kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador.
Van Gaal amewahi kuongeza klabu kubwa za dunia, hivyo beki huyo wa kati ambaye hatakuwepo Old Trafford msimu ujao baada ya kutangaza kuondoka majira ya kiangazi mwaka huu amesema kocha huyo anaweza kuleta mafanikio katika michuano ya ligi kuu.
“Anaonekana mtu imara sana na muelekezaji. Ana uelewa na ufahamu mkubwa kwa kila anachotaka kufanya. Unatakiwa kuwa hivyo katika klabu kama Man United,” Ferdinand aliwaambia waandishi wa habari
“Katika klabu alizopita-Ajax, Bayern Munich, Barcelona- anaonekana kufanya mambo kwa falsafa yake na nadhani atafanya hivyo akiwa na Man United.
Van Gaal ataelekeza nguvu kubwa ligi kuu ya England katika msimu wake wa kwanza kwasababu Ma United walishika nafasi ya 7 na kushindwa kufuzu michuano ya Ulaya, na Ferdinand anasema mazingira hayo yatawafanya warudi kwenye mbio za ubingwa”.
Post a Comment