Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward (katikati) amesema klabu itakosa Pauni Milioni 30 kwa kutoshiriki michuano ya Ulaya
KITENDO cha Manchester United kushindwa kufuzu kushiriki michuano ya ulaya msimu ujao kutaitia hasara klabu hiyo ya Paundi Milioni 30, imeelezwa na mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo, Ed Woodward.
Woodward amesema licha ya kutokea hivyo, haitaiathiri Man United katika solo la usajili.
“Kutokana na mikataba ya Televisheni, tunakadiria tutakosa Pauni Milioni 30 za michuano ya Ulaya. Matarajio ya klabu yalikuwa ni kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa na sasa tutajipanga katika usajili wetu”.
Akizungumza katika mkutano wa simu, alisema: “Katika msimu wa 2013-14, tumemaliza vibaya katika nafasi ya saba, ambayo inamaanisha hatutashiriki michuano ya Ulaya.
“Kuwa na uhakika kila mmoja katika klabu anapambana kuhakikisha msimu ujao tunakuwa katika kiwango cha juu cha Manchester United.
“Tumefanya mabadiliko ya bench la Ufundi Aprili, tumefurahi kuwa na Ryan Giggs kwa kumalizia msimu vizuri. Kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu katika kupata kocha mpya na tarajia atatangazwa muda si mrefu,”.
Louis van Gaal ndiye kocha anayetarajiwa kuichukua Manchester United baada ya Fainali za Kombe la Dunia atakapoiongoza kwa mara ya mwisho Uholanzi.
Jumatano Giggs alitua Uholanzi na akapigwa picha na inasemakana alikwenda kufanya mazungumzo na Van Gaal kwa niaba ya klabu.

Post a Comment