0
Kuna vitu ambavyo Bongo mara nyingi watu huwa hawafuatilii lakini kumbe upande mwingine ni big deal.
Kuna siku nimekutana na tshirt zenye picha za mastaa wa Bongo zikiwa zinauzwa kwenye duka moja town, sina uhakika kama ni kweli wasanii husika wanahusishwa kwenye biashara hii!
Story kutoka Uingereza, Mahakama ya rufaa London imetoa hukumu ya kesi ya madai kati ya Rihanna na duka la Topshop Arcadia ambalo linauza nguo, Rihanna aliwashtaki kwa kuuza nguo zenye picha yake bila kuwa na makubaliano yoyote na duka hilo.
Kesi hiyo ilitolewa hukumu mwaka 2013, wenye duka wakatakiwa kulia fidia ya dola laki 5 lakini wakakata rufaa ambayo kwenye hukumu ya Mahakama ya rufaa, Rihanna kashinda tena.
 Hii ni moja ya Tshirt yenye picha ya Rihanna
 Hapa ilikuwa story ya Rihanna baada ya kushinda kesi mwaka 2013, unaweza kuicheki.


 Picha iliyotumiwa kwenye nguo hizo ilichukuliwa wakati Rihanna akifanya video ya wimbo wake mwaka 2011.

Post a Comment

AddThis

 
Top