0
Mcheza tenisi namba moja duniani, Serena Williams amesonga katika raundi ya tatu ya michuano ya Australian Open kwa kumg’oa Vera Zvonareva raia wa Urusi.

Serena amemtoa Mrusi huyo kwa seti mbili mfululizo za 7-5 na 6-0.
Hata hivyo Zvonareva aliyewahi kuwa namba 2 kwa ubora kabla ya kuporomoka hadi 203, alionyesha upinzani mkali katika seti ya kwanza kabla Serena kucharuka katika seti ya pili.

Post a Comment

AddThis

 
Top