KIFARU ASISITIZA MTIBWA ITAITESA SIMBA NA KUBEBA UBINGWA
Mtibwa Sugar wametamba kuwa wataimaliza Simba kilahisi na kubeba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, keshokutwa.
Simba na Mtibwa Sugar zinakutana kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, keshokutwa.
Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ametamba kikosi chao kimekamilika kila idara.
“Wakati mwingine watu wajue namna ya kulinganisha, sasa unafananisha vipi Simba na Mtibwa Sugar? Angalia kwa takwimu.
“Walinzi bora wako Mtibwa, viungo bora wako Mtibwa na hata washambuliaji wakali wako kwetu. Sasa Simba watafanya nini?” alijigamba Kifaru.
Watu waje uwanjani Jumanne, wakishindwa wake kwenye runinga wao Simba wanavyoteseka.
Post a Comment