0
Jordan Henderson (wa pili kulia) na Diego Costa (kulia) pia walirushiana maneno walipokuwa uwanjani
JORDAN Henderson na Diego Costa wameripotiwa kuwa na ugomvi walipokutana nje ya vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la ligi iliyopigwa jumanne iliyopita kwenye uwanja wa Anfield baina ya Liverpool na Chelsea.
Wawili hao waliwakiana vikali na kutaka kupigana, lakini waliamuliwa na wahudumu wa vyumba vya kubadilishia nguo.
Inaaminika kwamba hawakurushiana ngumi, lakini wachezaji hao walisukuma kwa hasira na kurushiana maneno.

Post a Comment

AddThis

 
Top