Chama cha wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeitaka serikali kufanya marekebisho ya sheria inayoruhusu mwanafunzi mjamzito kufukuzwa shuleni ili ziendane na wakati uliopo na wanafunzi wanaopata ujauzito kupata fursa ya kuweza kuendelea na masomo na kupunguza idadi ya wanawake tegemezi kutokana na kukosa elimu.
Akizungumza katika mahojiano na East Africa Radio Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka amesema kuwa wanafunzi wajawazito wanafukuzwa shule kimakosa kutokana na sheria ya makosa ya jinai kutotaja kosa la ujauzito kama kosa la kimaadili hivyo kutaka kurekebishwa kwa sheria hiyo itakayotoa nafasi kwa mwanafunzi kujifungua na kuendelea na masomo.
Home
»
» Unlabelled
» Serikali Yaombwa Kurekebisha Sheria Inayoruhusu Mwanafunzi Mjamzito Kufukuzwa Shuleni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment