0
Na Mwandishi Wetu, Tabora
Unyama wa kutisha kisa utajiri! Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 (pichani jina linahifadhiwa), anadai kukatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Mashaka ili akauze Sh. milioni tano za Kitanzania akauze kwa mganga wa kienyeji ili apate mtaji.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe anayefahamika kwa jina moja la Mashaka.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo baya, mama huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete ambapo anadaiwa kukutwa na kisanga hicho hivi karibuni.
Mwanamke huyo anadai kujeruhiwa na mumewe usiku wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao Mtaa wa Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu akiwa wodini kwenye hospitali hiyo akiwa na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Siku ya tukio, nakumbuka mume wangu alikwenda kutembea, aliporejea nyumbani alifuatana na mtu mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji.

“Walipofika nyumbani aliniambia yupo na mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akitafuta viungo vya sehemu za siri za mwanamke akiwa na fedha milioni tano.

“Mimi nilikataa baada ya kunishawishi lakini usiku nilipokuwa nimelala, mume wangu alinikata huku akiniamuru nisipige kelele kwa kuwa alikuwa ameshapatana bei na kwamba ulikuwa ni utajiri mkubwa.”
Alisema baada ya tukio hilo alijikuta amelazwa hospitalini hapo hivyo hajui kama mumewe huyo alishakamatwa au la.

Kwa mujibu wa majirani zao, Mtaa wa Kazaroho, lilikuwa ni tukio la kutisha kwani wasamaria wema ndiyo waliomkimbiza mama huyo hospitalini ili kuokoa uhai wake.
Majirani hao walimtaka Waziri wa Maendeleo ya Wanawake Jinsia na Watoto, Sophia Simba kufanya kazi ya ziada ili sheria ichukue mkondo wake ili kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyoshamiri kwa kasi nchini.

Kwa mujibu wa mmoja wa madaktari hospitalini hapo ambaye hakutaka kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, mama huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini baadaye alipata nafuu hivyo anaendelea vizuri na matibabu.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Suzane Kaganda aliyehamishiwa mkoani hapa hivi karibuni hazikuzaa matunda hivyo zinaendelea.

Post a Comment

AddThis

 
Top